Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pongezi zangu kwa jeshi la Sudan, Natamani hali hii itokee kwenye ile Nchi ya AHADI.
Tatizo kubwa la hawa viongozi wa Afrika ni moja tu. Hata huyo atakayekuja naye utakuta anafanya madudu yale yale na hata mabaya zaidi. Miaka na miaka bara zima liko pale pale hakuna kwenda mbele japo kuna vi exceptions vya hapa na pale (naambiwa pengine Botswana na Rwanda). Tatizo lipo katika mfumo na falsafa ya kijumla. Mwafrika hajui nafasi yake ya kijamii, kimaendeleo na hata kiuchumi katika dunia hii. Hakuna anachofanya bila kuamriwa na wengine. Raslimali nyingi anazo lakini zinawanufaisha wengine. Wanaotawala lengo lao ni kujinufaisha wao na vibaraka wao wachache. Bara karibu lote linanuka ufisadi na ubinafsi wa kutisha wa viongozi.

Akina Albashir wataondoka. Akina Sassou Nguesso wataondoka. Akina Mobutu wataondoka. Akina Dos Santos wataondoka. Akina Nguema wataondoka...lakini hakuna kitakachobadilika as long as wale wanaokuja nao ni zao la mfumo na falsafa zile zile. It will just be their time to eat and business as usual.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…