Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ripoti zimekuwa zikidai kwamba Hazard anajipangaa kulazimisha uhamisho wa kwenda Real Madrid mwishoni mwa msimu huu ili kutimiza ndoto zake huku Chelsea wakiwa kwenye wakati mgumu wa kumzuia mchezaji huyo kama watashindwa tena kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
 
Hazard amekuwa kwenye kikosi bora kabisa msimu huu akifunga mabao 19 na kuasisti mara 12 katika mechi 42 alizoitumikia klabu hiyo ya London kabla ya mchezo wao wa usiku wa jana Alhamisi kwenye Europa Ligi.
 
Inadaiwa mastaa mbalimbali wanaokutana na Mwanamuziki maarufu wa Marekani, Drake wanajikuta wakifeli katika michezo yao inayofuata. Sergio Aguero amekuwa staa mwingine ambaye amekutana na laana ya mwanamuziki huyo.
 
Juzi Jumanne katika pambano la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, Aguero alikosa penalti iliyopanguliwa na kipa wa Tottenham, Hugo Lloris huku City wakichapwa bao 1-0 katika pambano la kwanza la robo fainali michuano hiyo.
 
Acha zipigwe, maana ni uwendawazimu kukubali kutawaliwa tena na jeshi.
 
Aguero alikutana na Rapa huyo maarufu wa Canada katika ukumbi wa Manchester Arena Machi 10 mwaka huu ikiwa ni siku moja baada ya City kuichapa Watford 1-0 katika pambano la Ligi Kuu ya England kwa bao la Riyad Mahrez.
 
Mwaka 2014, staa mwingine ambaye aliingiza timu yake katika majanga ni nyota wa Liverpool, Daniel Sturridge ambaye alikwenda katika shoo ya Drake jijini London lakini mwishowe kikosi cha Liverpool kilichokuwa chini ya kocha, Brendan Rodgers kilikosa ubingwa.
 
Bondia maarufu, Conor McGregor alikumbana na mkasa wa kudundwa katika pambano lake dhidi ya Khabib Nurmagomedov mwaka jana baada ya kufanyiwa promosheni na Drake kuelekea katika pambano hiyo. Hata hivyo McGregor alidundwa vilivyo na mpinzani wake huyo kutoka Russia. Shabiki mmoja wa Manchester aliposti picha ya Drake na kuuliza β€œMessi yuko wapi” akimaanisha kwamba angependa staa huyo wa Barcelona akutane na Drake kabla ya pambano la jana la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…