Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Bondia maarufu, Conor McGregor alikumbana na mkasa wa kudundwa katika pambano lake dhidi ya Khabib Nurmagomedov mwaka jana baada ya kufanyiwa promosheni na Drake kuelekea katika pambano hiyo. Hata hivyo McGregor alidundwa vilivyo na mpinzani wake huyo kutoka Russia. Shabiki mmoja wa Manchester aliposti picha ya Drake na kuuliza “Messi yuko wapi” akimaanisha kwamba angependa staa huyo wa Barcelona akutane na Drake kabla ya pambano la jana la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Tayari Manchester United iliwahi kukumbana na laana ya Drake. Staa wao wa kimataifa wa Ubelgiji, Romelu Lukaku alikwenda kukutana na mwanamuziki huyo mwezi uliopita Machi 13 na kupiga naye picha. Mechi iliyofuata United ilichapwa ugenini Wolves.
 
Mwanamichezo ambaye anajifanya jeuri na kutoogopa mzimu wa Drake ni bondia maarufu wa Ungereza, Anthony Joshua. Bondia huyu wa uzito wa juu ameshinda kila pambano katika mechi zake 22 zilizopita. Anajiandaa kupambana na Jarrell Miller mnamo Juni Mosi mwaka huu. Kuonyesha kwamba ni jeuri, Joshua alipiga picha na Drake wakati Rapa huyo alipotembea Gym yake mwezi uliopita na Joshua akatuma picha mitandaoni akilinadi pambano lake dhidi ya Miller kama ‘Pambano la kuvunja nuksi’.
 
a5c4157c3607289e2cf92413e1305fa0.jpeg
 
Anamaanisha kwamba ana uhakika wa kumtwanga Miller licha ya kupiga picha na Drake miezi miwili kabla ya pambano hilo linalotarajiwa kuwa kali na la kusisimua. Endapo Joshua atadundwa basi Drake atakuwa mtu wa kuogopwa kukutana naye. Kwa sasa Drake anakwenda zake Ubelgiji na Uholanzi katika ziara.
 
Ni wazi kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp atawapiga marufuku wachezaji wake wasikutane na kupiga picha na Rapa huyo ambaye umaarufu wake unaongezeka kila siku.
 
Supastaa wa Chelsea, Eden Hazard ameripotiwa ameshafanya uamuzi wake wa kwenda kujiunga na Real Madrid mwishoni mwa msimu huu, hivyo hakuna kitu ambacho wababe hao wa Stamford Bridge watakifanya asiondoke.
 
The Blues wanahangaika kumshawishi Hazard asaini dili jipya baada ya hili la sasa kufika tamati mwakani, lakini mpango huo huonekani kukamilika kutokana na mchezaji mwenyewe tayari ameshahamishia mawazo yake ya kwenda kucheza Bernabeu.
 
Madrid inaendelea kuhusishwa na mchezaji huyo, ambaye Chelsea hawatakuwa na ujanja zaidi ya kukubali tu kumpiga bei jambo itabidi wakubali yaishe kwa sababu Los Blancos hawapo tayari kutoa Pauni 100 milioni kupata huduma ya mchezaji huyo, ambaye mwakani tu mkataba wake utafika mwisho.
 
The tiger shark is the second most dangerous shark in the world. It is sometimes called the ‘garbage can of the ocean’ because this shark can eat anything and not only animals. This shark was once found earring a chicken poop with the remains of feathers and bones in its mouth.
Anapatikana bahari ipi
 
Back
Top Bottom