Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwanamichezo ambaye anajifanya jeuri na kutoogopa mzimu wa Drake ni bondia maarufu wa Ungereza, Anthony Joshua. Bondia huyu wa uzito wa juu ameshinda kila pambano katika mechi zake 22 zilizopita. Anajiandaa kupambana na Jarrell Miller mnamo Juni Mosi mwaka huu. Kuonyesha kwamba ni jeuri, Joshua alipiga picha na Drake wakati Rapa huyo alipotembea Gym yake mwezi uliopita na Joshua akatuma picha mitandaoni akilinadi pambano lake dhidi ya Miller kama ‘Pambano la kuvunja nuksi’.
 
Anamaanisha kwamba ana uhakika wa kumtwanga Miller licha ya kupiga picha na Drake miezi miwili kabla ya pambano hilo linalotarajiwa kuwa kali na la kusisimua. Endapo Joshua atadundwa basi Drake atakuwa mtu wa kuogopwa kukutana naye. Kwa sasa Drake anakwenda zake Ubelgiji na Uholanzi katika ziara.
 
T.I. on Why He's Going After Kodak Black Following Lauren London Comments: 'I See Myself in This'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…