Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

🤣🤣🤣🤣 jf buana
 
Real Madrid wanataka kulipwa kitita cha pauni milioni 112 ili kumuachia mshambuliaji wao raia wa Wales Gareth Bale, 29, mwishoni mwa msimu huu. Madrid wanaamini vilabu vikubwa vya Uingereza vitakuwa radhi kulipa fedha hizo. (AS)
 
Kocha wa Everton Marco Silva ametangaza kuwa huenda akawasjili moja kwa moja beki Kurt Zouma, 24 kutoka Chelsea, na kiungo Andre Gomes, 25 kutoka Barcelona - ambao wote wapo kwa mkopo klabuni hapo. (Liverpool Echo)
 
Silva pia amesema wala hajali uvumi unaoendelea kuwa kiungo tegemezi wa klabu hiyo na timu ya Taifa ya Senegal Idrissa Gueye, 29, kuwa atajiunga na Manchester United mwishoni mwa msimu. (Manchester Evening News)
 
Arsenal wanatariwa kuingia katika harakati za kumsajili kiungo wa Manchester United Ander Herrera, 29, kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu, na kupigana vikumbo na PSG juu ya saini ya Mhispania huyo. (L'Equipe, via Express)
 
Wakati huo huo, United wanapigiwa upatu kumsajili kiungo fundi wa klabu ya Sporting Lisbon Bruno Fernandes, 24, mwishoni mwa msimu. (A Bola, via Mail)
 
Real Madrid hawatakubali kumuachia beki wao wa kati Raphael Varane, 25, kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu pasi na kutolewa kitita cha pauni milioni 431. (AS)
 
Wachezaji wa Bayern Munich mshambuliaji Robert Lewandowski, 30, na winga Kingsley Coman, 22, walipigana wakiwa mazoezini Alhamisi asubuhi (Bild - in German)
 
Arsenal wanataka kumsajili kiungo wa Ufaransa Christopher Nkunku, 21, ambaye amegoma kuongeza mkataba na klabu ya PSG. (Le Parisien - in French)
 
Arsenal wanataka kumsajili kiungo wa Ufaransa Christopher Nkunku, 21, ambaye amegoma kuongeza mkataba na klabu ya PSG. (Le Parisien - in French)
 
Liverpool wapo kwenye mazungumzo ya kina na kampuni ya Nike kwa ajili ya mkataba wa utengenezaji wa jezi zao ambao thamani yake utazidi hata ule wa Manchester United na Adidas wa pauni milioni 750. Iwapo mkataba wa Liverpool utasainiwa utakuwa ndiyo mkubwa zaidi kwenye historia ya Ligi ya Premia. (ESPN FC)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…