Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1. CR7 anafunga tu robo fainali

Cristiano Ronaldo anafunga mabao yake pale inapohitajika kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Supastaa huyo wa Ureno anayekipiga Juventus msimu huu, Jumatano alifunga kwa kichwa kwenye sare ya 1-1 ugenini kwa Ajax. Jambo hilo limemfanya Ronaldo kufikisha mabao 24 kwenye mechi 21 alizocheza robo fainali Ulaya, huku Messi akiwa amefunga mara 10 tu. Kwa ujumla amefunga mara 125 katika mechi 161 za Ulaya.
 
MECHI za kwanza za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imepigwa wiki hii inayoisha na hakika lilipigwa soka la kiwango kikubwa sana. Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wote walikuwa mzigoni kutafuta matokeo kwa timu zao huku mechi hizo zikiacha kumbukumbu kibao ambazo hakika ungependa ufungashiwe na kuondoka nazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…