*LEGEVU KAMA BAMIA*
[emoji2398] *Dr Beatus Chikoti*
1.Khasimu bin Khamisi,
na Ramadhani Kapera
Mmewageuza fisi,
mikia wasio bora
Kwa kutumia mkasi,
tundu mkatia fora
Legevu kama bamia,
mikia kweli dhaifu.[emoji1787]
2. Walichovya kule Kongo,
utamu wamenogewa
Wakauchora mpango,
waendelee tobolewa
Wafurahia mchongo,
kwenye vichaka vya miwa
Legevu kama bamia,
mikia kweli dhaifu.[emoji1787]
3. Katerero gulioni,
utamu wameachia
Ilikuwa hadharani,
sote tumeshuhudia
Imewashukia soni,
sasa wapo wanalia
Legevu kama bamia,
mikia kweli dhaifu.[emoji1787]
4.Kagera sio wachoyo,
raha wanawapatia
Waliwakosha mioyo,
FIFA wakakimbilia
Simba hawasemi siyo,
bali huwakumbatia
Legevu kama bamia,
mikia kweli dhaifu.[emoji1787]
5. Mbele ya mkuu wa nchi,
tundu walitobolewa
na leo tena kwa mchi,
tundu limepanuliwa
Kweli afichaye uchi,
uzazi hupungukiwa
Legevu kama bamia,
mikia kweli dhaifu.[emoji1787]