Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

43ee263d800cbe4aeb529b4b67d5116e.jpeg
 
Mastaa wa zamani wa soka wakiongozwa na mlinzi wa zamani wa Manchester United, Gary Neville wamewachana vibaya mastaa wa Manchester United huku kiaina wakimtetea kocha, Ole Gunnar Solskjaer wakati huu United wakipoteza pambano lao la saba katika mechi tisa zilizopita.
 
Sihitaji kuwataja majina kila mtu anajua ni kina nani. Wapo katika magazeti kila siku, wapo katika mitandao ya jamii kila siku. Kama ni mchezaji na hauna tabia nje, sahau kuhusu kipaji chako.” Alisema Neville.
 
Everton, walikimbia kilomita nne zaidi ya United katika kipindi cha kwanza. Everton! Unawatazama hawa majamaa ambao ni wapinzani wakubwa wa Liverpool, wapo tayari kufia uwanjani na kusema kweli kwa wachezaji wa Manchester inakera kuwatazama. Nimechukia sana. bado namuamini Ole na kile anachotaka kufanya.” alisema Neville.
 
Wiki chache zilizopita niliwahi kusema kwamba mashabiki waliwahi kuwa upande wa Jose Mourinho lakini baadaye wakataka afukuzwe. Safari hii hawatataka Ole Gunnar Solskjaer afukuzwe. Nadhani itakuwa safari ya wachezaji.” Alimaliza Neville.
 
Nadhani kuna mkusanyiko wa wachezaji ambao akili yao ni kuondoka Manchester United na kuna baadhi yao ambao sio wazuri tu katika kiwango cha kuchezea Manchester United. Hilo ndio tatizo kubwa. Katika kikosi chake leo (juzi dhidi ya Everton) nimewaona wachezaji wengi wa namna hiyo,” alisema Jenas.
 
Back
Top Bottom