Kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne hatacheza mechi ya leo ya vigogo wa jiji hilo itakayofanyika Old Trafford, kwa mujibu wa kocha wake Pep Guardiola.
Kiungo huyo Mbelgiji alipata jeraha lake jingine msimu huu wakati alipolazimika kutoka uwanjani katika mechi ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Tottenham iliyoisha kwa vigogo hao wa Ligi Kuu kuibuka na ushindi.
Man City inaweza kukamata usukani wa Ligi Kuu na kuongoza kwa tofauti ya pointi moja iwapo itaibuka na ushindi kesho na itafanikiwa kutetea ubingwa iwapo itashinda mechi zake tatu za mwisho.
Pia Kocha Ole Gunnar Solskjaer alitumia muda mfupi na wachezaji akionyesha kuchukizwa na kiwango kibovu cha Man United katika mchezo huo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Goodison Park, Jumapili iliyopita.
Ingawa kocha huyo aliomba radhi kwa mashabiki, lakini alichukizwa na kitendo cha Man United kucheza chini ya kiwango na ameahidia kufumua kikosi hicho katika usajili wa majira ya kiangazi.
Ndani ya vyumba vya kuvalia nguo hali ilikuwa tete kwani kila mmoja alimtaja mtu aliyedhani alikuwa chanzo cha kupata kipigo hicho cha aibu tangu kocha huyo alipotwaa mikoba ya Jose Mourinho.
Hatukujitendea haki wenyewe ndani ya uwanja, klabu na mashabiki. Kocha alizungumza na maofisa waliongea ukweli,” alisema nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
Solskjear na msaidizi wake Mike Phelan walifanya kikao cha dharura ambacho kililenga kupangua kikosi na kuongeza nyota wapya katika usajili wa majira ya kiangazi.
Licha ya kusajiliwa kwa bei mbaya Pauni60 milioni akiwa ndiye mchezaji aliyetua kwa fedha nyingi Man City, lakini Riyard amekosa namba katika kikosi cha kwanza.