Hapo ndipo alipotoa kali na kutaka avae jezi yenye nambari 900 mgongoni, 9,000 kifuani na 90,000 kwenye kaptula. Alitaka namba 900 iwe katika maandishi ya Kiarabu na 90,000 maandishi ya Kigujerati (Kihindi).
Alisema mgongo wake uliipenda namba 9 kama alivyompenda mke wake na hakuwa tayari kupokea nambari nyingine. Baada ya mjadala mrefu alikubali kuvaa jezi namba 18, lakini alitumia namba 1 na 8 kuandika 1 na 8 huku alama ya kujumisha ikiwa katikati.
Hii ilifanya jezi yake kuwa na maandishi yaliyosomeka 1+8 na hivyo kuwa na jumla ya 9. Alipoulizwa kama angepigwa marufuku kutumia namba ya 1+8 alisema angevaa jezi yenye namba 10-1 na kwa hivyo jawabu ingekuwa 9.
Kama na hilo lingekataliwa angevaa jezi yenye maandishi ya “Nine” (9). Alisema alikuwa anafanya juhudi mke wake azae watoto tisa na akifa tarehe 10 au 21 ataomba mazishi yasubiri mpaka tarehe 9 ya mwezi unaofuata.
Zamorano) alienda Mexico mwaka 2001 na kuichezea America kwa misimu miwili na kustaafu kucheza soka la kulipwa akiwa na klabu ya Colo-Colo ya Chile mwishoni mwa mwaka 2003. Siku hiyo aliingia uwanjani tumbo wazi akiwa amechorwa nambari 9 na baadaye ndiyo akavaa jezi. Timu ya taifa ya Chile aliichezea mara 69 na kuifungia mabao 34.
Siku moja katika mchezo wa ligi ya Mexico aliwala chenga walinzi na akibakia na golikipa alisimama, akainama na kuubusu mpira na baadaye aliuchota ukampita golikipa juu ya kichwa na kwenda wavuni.
Negrete aliutoa mpira wavuni na badala ya kwenda katikati ya uwanja ili mchezo uendelee alimpa golikipa na kumtaka aubusu na kumwambia hauna makosa na aliyefanya kosa ni yeye kwa kuusukuma wavuni. Negrete alipoulizwa na waandishi wa habari kwa nini alijiamini kupita kiasi alisema:
Ninapokuwa uwanjani huhisi mimi ni dereva wa gari na wachezaji wa upinzani ni abiria wangu na wanapaswa kwenda ninakotaka kwa vile nimeshika usukani.” Tofauti na wachezaji wengi mashuhuri wa miaka ya 1950, Negrete alitumia muda mwingi kuchezea klabu ndogo na alianza soka la kulipwa 1980 akiwa na miaka 30 alipojiunga na Universidad Nacional ya Mexico.
Kila alipotaka kusajiliwa kama mchezaji wa kulipwa alisema bado alikuwa mtoto mdogo na kuwaomba waliotaka kumsajili wasubiri apevuke kiumri. Alipojiunga na Unervsidad akiwa na umri mkubwa aliulizwa kwa nini alikawia kucheza soka la kulipwa jawabu lake ilikuwa kali kama mashuti yake.
Alisema: “Hata nje ya uwanja wa kandanda wapo wanaofunga ndoa mapema na wengine wanakawia hadi wafikapo miaka 50 na zaidi. Uamuzi ni mapenzi ya mtu na siyo vizuri kumuingilia mtu katika mapenzi yake.
Ninaamini hata baadhi yenu baba zenu wamekawia kufunga ndoa.”
Alipoambiwa mchezo wa kandanda unahitaji nguvu za misuli ambazo huwa katika hali nzuri mtu anapokuwa kijana alisema: ”Kila kitu hakiwi mpaka ufike wakati wake. Hata katika uzazi wapo wanaozaliwa miezi saba, tisa au 10. Wengine hutaka kuendelea kubaki tumboni na ndipo mama hufanyiwa upasuaji”.
Alipostaafu kucheza soka la kiushindani alikuwa na miaka 40 na alisema labda akifikia miaka 50 atafikiria kurudi uwanjani kwani alikuwa anapumzika kwa muda.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.