Msimu huu zilifanikiwa kufikisha timu nne kwenye robo fainali ya michuano hiyo na sasa kuna timu mbili zilizotinga nne bora ya mikikimikiki hiyo ya kibabe kabisa huko Ulaya.
Manchester City imekuwa timu inayotamba kwenye Ligi Kuu England kwa siku za karibuni, lakini kitu cha kushangaza huko kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wamekuwa hawana maajabu yoyote, wakifika nusu fainali mara moja tu na msimu huu wameshindwa baada ya kutupwa nje na Tottenham Hotspur.
Man City wamekuwa wepesi sana kwenye michuano hiyo hata hiki kikosi cha Pep Guardiola chenye mastaa kibao nacho pia kimekuwa kikisuasua na kutokuwa na maajabu yoyote kwenye michuano hiyo ya Ulaya.
Sheria ya bao la ugenini ndiyo iliyowavusha Tottenham Hotspur mbele ya Manchester City kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na hivyo kutinga nusu fainali ya michuano hiyo
Hakika huo ulikuwa ushindi muhimu kwa kocha Mauricio Pochettino katika kikosi hicho ambapo Spurs ikaweka rekodi ya kufika nusu fainali ya pili kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya katika historia yao.