Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

PARIS Saint-Germain wamebeba tena ubingwa wa Ligi Kuu Ufaransa. Lakini, jambo hilo limemfanya beki wa kulia, Mbrazili Dani Alves, anayecheza timu hiyo kuweka historia ya kuwa mchezaji aliyenyakua mataji mengi zaidi kuliko yeyote katika dunia ya mchezo huo.
 
Kutokana na hilo, Alves aliyewahi kucheza Barcelona na Juventus anawaongoza mastaa kibao kwa kunyakua mataji mara nyingi ikiwamo hawa watano bora kabisa orodha inayowahusu mastaa wawili wa kutoka Afrika na Wabrazili wawili huko Mhispaniola akiwamo mmoja, fundi wa mpira, Andres Iniesta.
 
5. Ibrahim Hassan -mataji 37

Gwiji wa Misri, Ibrahim Hassan amebeba jumla ya mataji 37 katika zama zake alizokuwa mchezaji kwenye klabu yake na timu ya taifa. Kwa muda mwingi wa soka lake, Hassan alicheza kwenye nchi yake ya Misri, huku akiicheza timu yake ya taifa mara 125 na kwenda kutamba katika kikosi cha Al Ahly katika zama mbili tofauti.
 
Beki huyo wa kushoto, ambaye kwa sasa ni mkurugenzi msaidizi wa michezo kwenye kikosi cha Paris Saint-Germain amebeba mataji 37 makubwa baada ya kupita kwenye vikosi matata kabisa, Ajax, Inter Milan, Barcelona na PSG, ambako kote alitamba na kubeba ubingwa wa michuano mbalimbali na hivyo kumfanya aingie kwenye orodha hii ya wakali waliojibebea mataji mengi kwenye soka la dunia.
 
3. Andres Iniesta -mataji 37

Bila shaka, Andres Iniesta kumbukumbu zake kwenye soka la ushindani anatambulika kama mmoja wa viungo bora kabisa waliowahi kutokea katika mchezo wa soka. Staa huyo alipokuwa kwenye kikosi cha Barccelona hakika alikuwa hakamatiki ndani ya uwanja na ndiko alikobeba mataji yake mengi pamoja na yale mengine aliyonyakua akiwa na timu ya taifa ya Hispania
 
Kwenye historia yake, Iniesta amebeba mataji 37 makubwa na hivyo kuwa mmoja wa wachezaji walionyakua mataji mengi duniani, huku moja ya mataji hayo ikiwamo Kombe la Dunia na ubingwa wa Ulaya huku Barcelona ikimpa mataji kibao ya La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa miaka yake 16 aliyodumu kwenye timu hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…