Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kinga hii ya kijamii imekuwa inatumika sana na wafanyabiashara kwenye matangazo, wanakuambia kila mtu anatumia kitu hiki, hivyo unaposikia kila mtu anatumia, unapata uhakika kwamba hata kama utakosea, hukosei peke yako.
 
Hatua ya kuchukua; acha kufuata kundi na fanya maamuzi kwa kutumia akili yako mwenyewe. Kitu hakiwi sahihi kwa sababu kila mtu anafanya, na mara nyingi kinachofanywa na wengi huwa siyo sahihi. Usiogope kuwa tofauti na wengine, simamia ukweli na fanya kilicho sahihi, bila ya kujali wengine wanafanya nini.
 
Tuna tabia ya kutii mamlaka na kufanya kile ambacho mamlaka zinasema ufanye, hata kama siyo sahihi. Mamlaka hizi ni kuanzia ambazo ni ndogo mpaka kubwa. Mfano wazazi ni mamlaka kwa watoto, madaktari, walimu, viongozi wa kidini ni mamlaka kwa wengi.
 
Wengi wanapokuwa hawana uhakika wa nini wafanye, huwa wanatii mamlaka na kufanya kile ambacho mamlaka inasema wafanye, hata kama siyo sahihi. Pia tumekuwa tunawaamini sana wale ambao wanatuambia ni wataalamu waliobobea kwenye eneo fulani, na tunachukua maneno yao kama ukweli usiohitaji kuhojiwa.
 
Hatua ya kuchukua; tenganisha mamlaka na kile kinachosemwa au kushauriwa, kihoji chenyewe bila ya kukiweka kwenye mamlaka husika ili uweze kuona kama ni kweli au siyo kweli, sahihi au siyo sahihi. Mara nyingi wenye mamlaka wamekuwa wanakosea, pia watu hao huwa wanakuwa na maslahi yao binafsi, hivyo fikiri kabla ya kuamua.
 
Kupata sababu.
Huwa tunapenda kupata sababu ya kila kitu kinachotokea, hatuwezi kutulia kama hatujapata sababu. Na hata kama hakuna sababu ya kitu kutokea, basi huwa tunatengeneza sababu zetu wenyewe, ili tu tuwe na uhakika wa nini kimesababisha.
 
Na kwa mambo yaliyotokea nyuma ni rahisi kukusanya sababu zilizopelekea yatokee kuliko kutengeneza sababu ya vitu vitakavyotokea. Sababu nyingi tunazojipa za mambo kutokea siyo sahihi. Tumekuwa tunahusianisha vitu visivyokuwa na uhusiano kwa sababu tu vimetokea kwa pamoja.
 
Na kwa mambo yaliyotokea nyuma ni rahisi kukusanya sababu zilizopelekea yatokee kuliko kutengeneza sababu ya vitu vitakavyotokea. Sababu nyingi tunazojipa za mambo kutokea siyo sahihi. Tumekuwa tunahusianisha vitu visivyokuwa na uhusiano kwa sababu tu vimetokea kwa pamoja.
 
Kuheshimu sababu.
Uhitaji wetu wa kupata sababu ya kila kitu, umepelekea sisi kuamini sababu ambazo siyo sahihi. Mtu anaweza kuwa anataka umpe kitu, ambacho kwa hali ya kawaida usingempa, lakini anapokupa sababu kwa nini anataka umpe, wewe unampa. Siyo kwa kuwa amekupa sababu sahihi, ila tu kwa kuwa ana sababu. Tuna tabia ya kuheshimu sababu hata kama siyo sahihi, na hii imekuwa inatumika na wengine kupata vitu kutoka kwetu
 
Hatua ya kuchukua; usikubaliane na kila sababu ambayo watu wanakupa, badala yake angalia uhusiano huo na kile ambacho watu wanataka. Mara nyingi utagundua hakuna uhusiano kabisa. Pia unapotaka watu wafanye kitu, wape sababu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…