Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

a7ff3fd55d64499a12a33ba9270dde39.jpeg
 
Makosa mengi kwa pamoja.
Hapa tumeona kosa moja moja tunalofanya kwenye maamuzi, lakini mara nyingi makosa haya hayatokei yenyewe, badala yake huwa yanaandamana pamoja. Na kadiri makosa mengi yanapokuwa pamoja, ndivyo tunavyoishia kufanya maamuzi mabovu kwenye maisha yetu.
 
Mfano kwenye wizi, mtu anaweza kuiba kitu kwa mara ya kwanza, kama hataadhibiwa basi ataendelea kuiba tena na kwa kuwa alishaanza kuiba basi anaendelea na wizi na wengine wanapoona mwenzao anaiba, wanaona ni sahihi na hivyo wanaiba pia. Hii inapelekea wale wanaoiba kuonekana wapo sahihi na wasioiba kuonekana hawapo sahihi.
 
Hatua ya kuchukua; kwenye kila maamuzi na hatua tunazochukua, tuchunguze kwa kina msukumo wa sisi kufikia maamuzi hayo na kuchukua hatua ambazo tumechukua. Tunapogundua kwamba makosa mengi ya kisaikolojia yamehusika, tunapaswa kufanyia kazi kosa moja moja ili baadaye tuweze kufanya maamuzi bora zaidi.
 
hayo ndiyo makosa 28 ya kisaikolojia ambayo yamekuwa yanakusababisha ufanye maamuzi mabovu. Kwa kila maamuzi unayochukua kwenye maisha yako, jitafakari katika makosa haya ili usifanye maamuzi mabovu.
 
Back
Top Bottom