Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.
Screenshot_20190501-195810.jpeg
 
Sherekea ushindi mdogo mdogo.
Badala ya kusubiri mpaka ufikie lengo kubwa ndiyo usherekee, gawa lengo hilo kwa hatua utakazochukua kila siku kisha sherekea pale unapokamilisha hatua hizo. Hili litakupa furaha kila siku kwa kukamilisha hatua hizo ndogo.
 
Gawa lengo kubwa kwenye hatua ndogo ndogo.
Badala ya kuliendea lengo kwa ukubwa wake, ligawe kwenye hatua ndogo ndogo na kila unapomaliza hatua moja, unapata furaha na kupata msukumo wa kupiga hatua ya juu zaidi.
 
Kwa jukumu kubwa ambalo ni gumu kufanya, ligawe kwenye muda mfupi mfupi.
Kila mtu huwa ana jukumu kubwa analotaka kufanya, lakini hawezi kulianza kwa kuwa ni kubwa na gumu, hivyo anaishia kuliahirisha kila mara. Tenga muda mfupi mfupi wa kufanya jukumu hilo na anza. Mfano weka dakika kumi tu za kufanya jukumu hilo kisha fanya kwa dakika hizo kumi. Kwa njia hii utaanza kuchukua hatua na dakika kumi zinapoisha unakuwa unajisikia vizuri kuliko ulivyoanza.
 
Endelea kuongeza ugumu wa hatua unazochukua.
Kama ilivyo kwenye madawa ya kulevya, ukitumia kiwango kile kile, furaha huipati tena. Kadhalika kwenye kuchukua hatua ndogo ndogo, kama hatua unazochukua ni zile zile na zimeshakuwa rahisi kwako kiasi cha kuweza kufanya bila hata ya kufikiri hutapata tena furaha unapokamilisha. Badala yake ongeza ugumu kwenye kila hatua inayofuata, na unapovuka ugumu huo unapata furaha kubwa.
 
Cheka.
Kucheka kunazalisha kemikali ya endorphin ambayo inakuletea furaha. Kuwa na njia za kukuwezesha kucheka kila siku na utakuwa na maisha ya furaha. angalia, sikiliza au soma vitu vinavyochekesha na ucheke.
 
Back
Top Bottom