Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema Mengi ni mmoja kati ya watu waliotoa mchango mkubwa kwenye masuala ya siasa na kifo chake kimeacha alama kubwa.
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amesema msiba wa Mengi ni mzito na hauelezeki kutokana na mchango mkubwa alioutoa mfanyabiashara huyo wakati wa uhai wake.
Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Salma Kikwete amesema Mengi ameacha pengo kubwa na atakumbukwa kwa mambo mbalimbali ikiwamo kujitolea kuwasaidia wanafunzi wanaosoma katika shule za sekondari zinazomilikiwa na Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake (Wama).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira ), January Makamba amesema ni msiba mzito na wamepoteza mdau muhimu kwenye sekta ya mazingira.
"Tumempoteza mtu muhimu mchango wake ulikuwa mkubwa hasa katika kuvitumia vyombo vyake vya habari kutoa elimu. Tupo pamoja katika msiba huu," amesema Dk Makakala.