Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuanza biashara kutoka kiwango cha sifuri siyo kazi rahisi. Kama mjasiriamali utakutana na changamoto nyingi. Hili haliwezi kuwa tatizo ikiwa uko tayari kujifunza kutokana na makosa na kufahamu njia za kuyaepuka huko mbeleni.
 
Hivi ndivyo wajasiriamali wengi wanavyojifunza na kukua. Unapokuwa kwenye biashara ni lazima ufahamu makosa ambayo yanaweza kuathiri biashara au uwekezaji wako; ili ujitahidi kuyaepuka ama kuyapunguza kadri iwezekanavyo.
 
1.Kujifanya unafahamu kila kitu

Usijifanye unajua kila kitu, hasa kama ndiyo umeingia kwenye ulimwengu wa kibiashara. Kwanini? Kwa sababu kuendesha biashara ni kujifunza na kupata uzoefu. Jitahidi kujifunza na kujijengea uzoefu kupitia maarifa mbalimbali ili uweze kuendesha biashara yako vyema kama mjasiriamali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…