Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.
FB_IMG_1557225883238.jpeg
 
Kuanza biashara bila miundombinu

Ni dhahiri kuwa wengi husema “mwanzo ni mgumu” lakini ni lazima utengeneze miundombinu kadhaa. Unapoanzisha biashara kama mjasiriamali jitahidi kuweka miundombinu kadhaa ya muhimu kwanza kabla hujaanza kufanya biashara.
 
Kuendesha biashara kunahitaji vifaa na rasilimali kadha wa kadha ambazo ni muhimu ziandaliwe kabla. Miundombinu hii inaweza kuhusisha mtaji, vifaa muhimu, ofisi ndogo ya kuanzia, n.k Kumbuka hivi ni vile vitu vya msingi tu na siyo mbwembwe zisizokuwa na msingi.
 
Kutazama mafanikio pekee

Biashara yako au mradi hauwezi kukua ikiwa mipango yako haibadiliki. Wewe kama mjasiriamali unatakiwa ufikiri kwa upana unapokuwa unafanya maamuzi. Kutazama tu mafanikio bila kuzingatia ubora wa huduma ni kujizamisha majini wewe mwenyewe. Ni dhahiri kuwa kuzingatia kumudu kuwa na ubora wa huduma pamoja na ukuaji wa biashara ni jambo zuri zaidi.
 
Kutaka wateja wakutafute

Je ni kweli kuwa unataka wateja wakutafute na wakati soko limejaa wajasiriamali wengine na huduma? Hapana! Kama unataka kukuza msingi wako wa wateja ni lazima uwe pale ambapo wateja wapo. Kwa kufanya hivi watakutambua na kununua huduma au bidhaa yako.
 
Kupuuza nafasi ya teknolojia

Wajasiriamali wengi wa Kiafrika wanadhani kuwa teknolojia ni kwa ajili ya wazungu au kampuni kubwa. Haijalishi ni biashara au mradi gani unaoufanya ni lazima uzingatie nafasi ya teknolojia. Teknolojia iko kila mahali; hivyo ni vyema ukatumia teknolojia kama vile intaneti kutangaza, kuuza, na hata kuwasiliana na wateja wako.
 
Matumizi mabaya ya fedha

Watu wengi hawana matumizi mazuri ya fedha hasa wao binafsi. Tatizo hili limekuwa pia likijitokeza pale mtu anapotakiwa kusimamia na kutunza pesa za mradi au biashara.
 
Back
Top Bottom