Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa mfano zamani watu walinunua zaidi kuku walio hai, lakini leo soko la kuku waliochinjwa ni kubwa pia; kwanini wewe bado unauza tu kuku walio hai? Ni dhahiri ukitazama mfano huu utaona jinsi kosa hili linavyowaathiri wajasiriamali wengi katika maeneo mbalimbali.
 
Kushindwa kubaini wateja lengwa

Ni lazima wewe kama mjasiriamali uwabaini wateja wako ili huduma au bidhaa yako iuzike. Kwa mfano umetengeneza dawa ya kuua mbu, kisha unaiuza mikoa ya baridi badala ya mikoa yenye joto (kwenye mbu wengi)
 
ni dhahiri kuwa hutoweza kupata wateja wa bidhaa yako sawa sawa. Chukua hatua leo watafute na uwafuate wateja sahihi wa huduma au mradi unaoufanya.
 
Mbinu duni za masoko

Maswala ya masoko ni taaluma kamili ambayo watu hujifunza katika shule na vyuo mbalimbali. Hivyo ni muhimu wewe kama mjasiriamali kutokupuuzia taaluma hii kwani ndiyo itakayokuwezesha kubaini njia bora na sahihi za kuuza huduma au bidhaa yako.
 
Hakikisha mbinu za masoko unazifahamu vyema tena zinaendana na soko husika la bidhaa yako. Hakikisha pia mbinu zako zinabadilika kulingana na mazingira na hali ya soko.
 
Maarifa sahihi ni msingi wa kufanya vitu kwa ubora. Ni dhahiri kuwa makosa mengi yaliyoelezwa hapa yanatokana na ukosefu wa maarifa stahiki ya ujasiriamali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…