MANENO YA BABA ASKOFU DR BENSON BAGONZA BAADA YA TAARIFA ZA KUTEKWA MDUDE
Ukinyamaza, watachinjwa; wakiwamaliza, utachinjwa.
Ukipiga kelele, watachinjwa; wakiwamaliza, utachinjwa.
Wakitumaliza, watachinjana;
Atakatebaki, atajichinja.
Akijichinja, hatazikwa; KWA HIYO,
Kukaa kimya; kupiga kelele;
Kuchinja na kuchinjana;
Yote mwisho wake ni ibada ya sanamu. Uhai wa wapiga kelele, wakaa kimya, wachinjaji na wachinjwao, umo mikononi mwa aliyechinjwa msalabani.
Wakijua tutafufuka naye, wajiandae kuishi na waliyemuua. Msiogope, HAYUPO AMEFUFUKA, AMETANGULIA KWENDA GALILAYA.