Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Neymar ambaye siku takribani 11 zilizopita aliingia matatani baada ya kuonekana akimpiga ngumi shabiki, anadaiwa kurushiana maneno makali na Draxler kwenye chumba cha kubadilishia nguo baada ya timu yake kupokea kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Montpellier, Aprili 30.
 
Baada ya kichapo hicho, Draxler anadaiwa kutoa maneno ya ukali kwa wachezaji wenzake akiwatuhumu kufanya uzembe uliopelekea wapinzani wao kusawazisha mabao mawili na kupata la ushindi, kitendo ambacho kilimkera Neymar ambaye aliamua kujibizana na kiungo mshambuliaji huyo.
 
Wewe ni nani hadi uniambie maneno kama hayo? Mtu mwenyewe unapiga pasi za kurudi nyuma tu!’, Neymar aliongea kwa hasira kujibu Draxler jambo lililotaka kuibua mzozo baina yao ingawa ulitulizwa kabla haujapamba moto.
 
Matukio hayo ya utovu wa nidhamu wa mfululizo ambayo yamekuwa yakifanywa na Neymar, yameendelea kutokea katika kipindi ambacho wengi wanamkosoa Neymar kwa mchango duni anaoutoa ndani ya kikosi cha PSG licha ya yeye kuwa ndio mchezaji mwenye thamani kubwa kikosini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…