Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baadhi ya mashabiki waaamini kwamba Hazard hatasaini dili jipya kwenye timu yao, isipokuwa ataendelea kubaki hapo Stamford Bridge ili kuokoa Pauni 100 milioni za Real Madrid, ambapo atakapokwenda kujiunga nao bure mwishoni mwa msimu ujao atakwenda kulipwa mshahara mara mbili ya kiwango anachovuna kwa sasa kwenye kikosi cha The Blues. Kama Hazard akibaki Chelsea atakuwa na ruhusa ya kusaini mkataba wa awali na Real Madrid itakapofika Januari mwakani.
 
Herrera alitua Man United mwaka 2014 akitokea Athletic Bilbao na katika miaka mitano aliyokuwa kwenye kikosi cha Old Trafford, ameshinda taji la FA Cup, Kombe la Ligi na Europa League na alishinda tuzo yenye thamani ya Sir Matt Busby inayotolewa kwa mchezaji bora wa mwaka katika msimu wa 2016/17.
 
Na sasa kiungo huyo Mhispaniola anajiandaa kujiunga na Paris Saint-Germain kwa uhamisho wa bure. Kilikuwa kitu cha chinichini kuhusu Herrera kwenda kujiunga na PSG, lakini sasa jambo hilo lipo wazi baada ya Man United kuweka video ya mchezaji huyo kwenye ukurasa wao wa Twitter.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…