Polisi mkoani Tabora inamshikilia mkazi wa Malolo, Mwanjaa Salum (47) kwa tuhuma za kumuunguza mtoto wa kaka yake (miaka mitatu) kwa madai ya kukojoa kitandani.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Emmanuel Nley, akizungumza leo Mei 16, 2019, amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 13, 2019 baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa raia mwema.
Amebainisha, “baba wa mtoto aitwaye Yusufu Hassan, baada ya dada yake kumfanyia ukatili mwanawe huyo, pengine kwa lengo la kumlinda dada yake aliamua kumpeleka kwa mama yake mzazi eneo la Ng'ambo, Manispaa ya Tabora.”
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.