Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema video ya ngono iliyosambaa mitandao juma lililopita ikidaiwa ni ya Askofu Josephat Gwajima, ni ya kutengenezwa, na kwamba hadi sasa watu wawili wanashikiliwa na Polisi. Aidha, ameeleza kuwa uchunguzi wa sakata hilo bado unaendelea.