Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Zanzibar ilihitaji sauti kama ya DUP katika bunge ili kuweza kusimamia yale yenye maslahi nasi. Wabunge 10 wa DUP wanaweza kuiangusha serikali ya Muingereza kwa sasa kutokana na makubaliano yao hasa kwa vile chama kinachoongoza nchi hakina wingi wa maamuzi. Sifikirii kama utamsikia akina Kesi wa Nkasi au Waziri kudharau mamlaka, madai au hoja za upande wa Zanzibar pale mfumo wetu utapobadilika na kutoa uhuru wa namna hii. Mifumo hii inajenga heshima, usawa na haki baina ya pande husika badala ya mkubwa kutazama yenye maslahi naye kwanza akidharau wengine kwa udogo wao.
 
. Tusome kwa wenzetu namna ya kutafautiana kwa hoja bila ya vitisho, hasama na kukomoana. Siasa ni ushindani wa hoja na ridhaa ya walio wengi. Unaiona nchi yao ilivyo katika mgogoro lakini hawayumbi kiuchumi, kisiasa wala kijamii. Hutasikia mbunge wao kumiminiwa risasi kwa kumkataa mkuu wa nchi, hutasikia watu wasiojulikana wakikamata wanaharakati wanaopinga ajenda ya serikali au mkuu wa nchi. Neno moja la kulitafsiri ni “Civilisation” tujiulize tumekosea wapi?
 
Heshima ya Urais na ukuu wa nchi si jeshi bali Bunge. Hapa kwetu katika bunge la katiba wapo waliotamani kuingia msituni kwa kuona tu upana wa demokrasia ulivyopea nchini. Hakutakuwa na Rais mwema ambae habebi ridhaa ya wabunge huru katika nyoyo zao. Hakuna aliejuu kati ya wenye kubeba mihimili ya nchi. Serikali itafanikiwa pale haki, uhuru, heshima na usawa utapobebwa na mihimili yote mitatu badala ya mmoja na ashki yake ya kutawala atakavyo.
 
Kinyume cha UTU ni UKATILI. Hakuna msamiati wa katikati baina ya utu na ukatili. Ima utakuwa na utu au utabaki katili. Kama Ilivyo haki na batili. Kinyume cha haki ni batil, huwezi kuwa mtenda haki lakini umejawa na yenye batil, viwili hivi haviendani.
 
Tuendelee na hii homa ya mikopo ya China kwa nchi masikini na namna gani madeni haya yameanza kuzaa maradhi mapya ya nchi mdaiwa kupoteza sehemu ya ardhi au mashirika yake kwa mdai. China imesoma mengi katika kipindi cha ukoloni wa Muingereza katika miaka ya 1800 na pamoja Ureno katika sehemu za Macau. Yanayotokea sasa yanaendana na historia yake ilipotoka na ndoto yake inapotaka kuelekea.
 
Kuelewa vyema haya yanayotokea kuanzia Zambia, mpaka Sri Lanka basi rudi nyuma katika historia ya ubwebwaji wa Hong Kong na Muingereza pamoja na Macau kwa Mreno. Tafauti utaikuta ni namna tu ya matukio ya ubwebwaji wenyewe lakini ramani ndio ile ile ya mdaiwa dhaifu dhidi ya mdai mwenye nguvu alieamua kujikodisha ardhi kufidia madai yake. Wimbo hapa ni mwenye nguvu na madai yake dhidi ya dhaifu, mdaiwa.
 
Hong Kong ilichukuliwa na Muingereza kama sehemu ya makubaliano ya kuzuia kuendelea kwa vita baina ya China na Falme ya Muingereza. Vita hivyo vilikuja kutokana na ufalme wa Qing kuzuia biashara ya Opium iliosimamiwa na Muingereza na matokeo yake baada ya China kuonekana kushindwa katika vita hio ndio ukaja mkataba wa Nanking uliotoa maelezo kwa Muingereza kulipwa na China fidia ya vita na biashara iliozuiwa.
 
Halkadhalika Uingereza ikapewa HongKong mkataba wa kukodishwa ardhi hio kwa miaka takriban 100. Ukitazama kwa undani utakuta yaliotokea kwa Sri Lanka na bandari yake ilioikabidhi China kufidia madeni ni yale yale ambayo China ilikumbana nayo dhidi ya Muingereza tafauti ikiwa wakti ule nguvu iliotumika ni ya mizinga na jeshi na kwa sasa ni mikopo isiolipika. Sri Lanka anadaiwa dola bilioni nane na mchina, katoa bandari kwa miaka 100 apate afuweni.
 
Ukitazama pia Macau nayo hadithi ndio hii hii ya mikataba ya kukodishwa kwa miaka 100 katika zama za ukoloni ambao China nae alikuwa mmoja wa waathirika wakubwa. Ureno iliingia kinyemela Macau, ikaweka mikakati yake iliozaa mikataba hii ya kujinyakulia ardhi na kuzitangaza sehemu husika kuwa ni milki ya taifa lake.
 
Kikubwa katika nyang’anya nyang’anya hizi ni sehemu husika na urahisi wake katika biashara zilizozifanya nchi husika kuwa tajiri na kubeba heshima ya kuogopwa. Kwa Hong Kong, mkataba wa Nanking uliwapa haki Uingereza ya kuendelea na biashara zao bila ya mitikiso ya mchina huku wakiwa sasa na bandari ya kimkakati kiulinzi na kiuchumi katika kulinda maslahi ya ufalme wao na taifa lao.
Na kwa Ureno, uwepo wao Macau ulirahisisha ile “route” kutoka Lisbon, Goa, Macau na Japan ambako biashara kubwa zilihakikisha ufalme wao unazidi nguvu na kunufaika. Sawa na bandari ya Sri Lanka kiusalama na kiuchumi kwa China au Zambia ambayo China inamaslahi makubwa Afrika nzima.
 
Katika athari nyengine za kunyakuliwa kwa ardhi hizi katika kilichoitwa kama “99 Years Lease” ni utumwa. Kwa Macau, wako wachina waliokamatwa na kupakiwa katika majahazi kupelekwa Cuba na sehemu nyengine za makoloni yao wakiwa watumwa kama ambavyo waafrika walivyofanywa.

Unapompa mtu mwenye nguvu kubwa ya kiuchumi na kiusalama haki ya kubeba kipande cha ardhi yako unakaribisha pia uonevu kwa wananchi wako waliopo sehemu husika. Mfano kwa Sri Lanka ambako bandari na miradi yote ya mikopo ya mchina ilisimamiwa na wenyewe ikiwa pamoja na wafanyakazi kiasi kwamba kuna kipindi Sri Lanka ilibeba wachina takriban 25000 kwa ajili ya kusimamia miradi yao. Wazawa wamefaidika vipi? Suala zito lisilojibika kirahisi, madeni yamebaki na mradi umekwenda kwa mkopwaji.
 
Ukitazama kwa sasa Zambia ambayo inaonekana tayari imepoteza shirika lake la umeme na mengine yakitajwa kufuatiwa ikiwamo mashirika ya habari basi unaanza kuelewa athari kubwa inayoinyemelea Afrika katika zahma hizi za mikopo isio na tija. Tunarudi kule kule katika zahma za ukaburu wa Afrika Kusini huku tukiwa vipofu wa kuelewa miaka 100 inaweza kugeuza sehemu zetu wenyewe kuwa na umiliki wa wengine hata wanapomaliza muda wao kama ambavyo HongKong na Macau ilivyo sasa katika “one country two systems” ya China hata ikiwa haijaridhika nayo. Tunakokwenda na madeni ni kugumu zaidi ukitazama kwa undani na athari za muda mrefu.
 
Tatizo kubwa la sisi waafrika ni ukaidi na kiburi katika kufanya maamuzi yanayobeba unafuu wa haraka lakini si endelevu. Hii mikopo inayobebwa kiholela inaishia kutuzidisha katika dimbwi la umasikini na kwa sasa tunaelekea katika si kufilisiwa tu bali kuporwa kidogo kidogo hata ile heshima ya kujiita tuko huru kujiendesha. Afrika isome kuwa maendeleo yanaanza kwanza kwa kujenga misingi imara ya haki kama “Pyramid” ilivyo.

Bila ya haki tutaishia kukopa, na fedha kuishia katika miradi isio na maslahi nasi kimkataba au wajanja wachache kujinufaisha wenyewe binafsi. Tutasoma lini athari za papara ya madeni?
 
Tunawaachia vizazi vijavyo ufukara mwengine wa mikopo na madeni holela na kidogo kidogo wanaweza kujikuta katika dimbwi la ukoloni mambo leo na utumwa mpya wa ulipwaji wa madeni yalio na riba isiokwisha. Maendeleo gani ambayo yatasimama na utu ikiwa asilimia 80 ya wananchi ni masikini wasio na uhakika wa pakulala na kula?

Maendeleo gani ya kweli ikiwa heshima, utu na haki ni tegemezi kwa mtoaji badala ya uhuru wa kuwapo kwa kila mwananchi? Lazima tujenge taasisi madhubuti katika haki ili uwekezaji usiwe na chembe ya shaka katika maslahi ya nchi kwanza na watu wetu badala ya kukurupuka na ushamba wa madaraka wa kutaka makubwa yasioendana na hali halisi ya maisha yalivyo.
 
Ukisikiliza hotuba za uongozi wa muhula huu basi kwa urahisi unaweza kuyasikiya yafuatayo:-
  1. Lack of attention to details : ukosefu wakuelewa. Mfano: Hata mwenye charahani mbili nae ana kiwanda.
  2. Narcism: kujipenda na kujitukuza. Mfano nikifufuka nitakuwa kiongozi wa malaika. Au mimi ndie mzizi mkuu, mimi jiwe.
  3. Unstable on truth: kutoaminika. Mfano kesi ya makenika na mabilioni yatayonunua kwa kila mtu Noah moja. Au Ukabudi wa Rais na mamlaka alionayo/asiyonayo kwa JMT au Dodoma kukusanya kodi zaidi ya Dar.
  4. Lack of empathy: ukosefu ufahamu wa hisia. Mfano kwa nini kila naqama kwenu tu, Mwafa! Mna njaa kwani mimi mpishi, mimi chizi na nimechagua chizi katika Wizara yangu.
 
Ni sawa na mchezo wa kuigiza tu. Msingi wa mwanzo wa uongozi wa umma ni ukweli. Sasa mtu ambae amefoji jina kitaaluma atategemewa aongoze kwa utu, ukweli na umakini?

Tatizo si Bashite bali Mzizi Mkuu alieyalea maovu na kuyapigia makofi. Yaani muhula wa drama na maigizo. Ndio tukasema tunahitaji Haki Huru sio ashki ya mtu na uungu mtu.
 
Tupitie hii makala ya Bloomberg ya April 2018 inayoeleza athari kubwa za kuficha madeni na kupika nambari za kiuchumi zilizoikumba Jamhuri ya Congo pamoja na Zambia. Ina mengi ya kutukumbusha kuhusu uchumi na namna gani propaganda za kuficha madeni zinaweza kutuathiri wakati mzizi mkuu anaondoka na kuturudisha nyuma katika zama za “Stone Age”.
 
Zambia ni mzalishaji mkubwa wa madini ya Coper na katika uchunguzi wa Bank of America ambayo ni moja wa wakopeshaji wake, Imeonekana kuwa na mkopo wa siri wa zaidi ya dola bilioni kumi ambazo hazijahesabiwa na kuwezekana kuliongeza deni la asilimia 30 zaidi katika miaka mitano ijayo hasa kwa riba ukichanganya na deni la sasa linalobeba 1/3 la GDP. Kiufupi khofu ya madeni haya na hizi namba za kupikwa zinaweza kuzidisha deni kwa zaidi ya asilimia 50 ya GDP siku za mbele.
 
Congo ni miongoni mwa wazalishaji wa mafuta, nayo imekumbwa na kadhia ya kuficha baadhi ya madeni yake kiasi kwamba hata IMF imeshindwa nayo kutambua ukubwa wa madeni yake kabla ya kufanya maamuzi ya kuikopesha. Kwa Congo inasemekana wamepokea pesa ya bidhaa ambazo bado wanunuzi hawajapokea bidhaa na hivyo kuhesabika kama deni ambalo serikali imekuwa kimnya kuweka wazi. Unapochukua fedha za watu wanaotegemea huduma waliokwisha lipia basi nalo ni deni linalohitaji kuwekwa wazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…