Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wawekezaji wanasema hili suala kwa sasa si la Zambia na Congo pekee bali takriban Afrika nzima ambapo madeni yanayohesabiwa ya asilimia 30 ya GDP yamekuwa makubwa kuzidi asilimia hamsini kwa sababu ya kukosekana uwazi na kufichwa fichwa kwa maelezo muhimu juu ya hali ya uchumi wa nchi. Matokeo yake ni nchi kutokopesheka na kutakiwa kulipa madeni kwa muda mrefu huku zikiyumba katika maendeleo na wananchi wakiumia zaidi.
 
Haya yaliwahi kutokea kwa Mozambique na yanaweza kutokea hapa nchini hasa ukitazama ishara za trilioni 1.5 ambazo hadi leo zimekosekana maelezo na huku akiachiwa mbeba propaganda kufikiri maneno kama “Hazijawiva” na kutukana wenye udadisi juu ya hali ya uchumi ilivyo itaitoa nchi katika balaa la kufilisika siku za mbele.
 
Ukitazama hapa kwetu utakuta thamani ya shilingi inayumba na dhaifu kwa upepo mdogo tu wa kimasingira. Benki zinafilisika na kumezwa na benki kuu, misamaha ya kodi kuanza kutangaziwa na majuzi benki kupunguza gharama za kukopa. Zaidi deni la nchi linaongezeka na bado tukidanganywa kuwa pesa zipo hata pale tunapoendelea kukopa kiholela.
 
Hakuna nchi huru inayotegemea msaada wa hali na mali wa bajeti yake. Uhuru unakuja na kujitegemea, sio ulishwe halafu useme niko huru. Wanaokufadhili lazima watakusema hasa unapokuwa dhaifu wa haki na utu. Watoe pesa za walipa kodi wao ili kukunufaisha wewe na uimla wako? Unataka kusimama na uhuru hebu kataa fadhila za hawa wanaokuingilia uhuru wako kwanza.
 
dhana nzima ya ujamaa imejaa wema lakini ni rahisi sana katika wema huo kupata wajanja wakaugeuza kuwa amri, nguvu na shurti bila ya utu na ubinaadam. Wengi wa wajamaa wamejawa na kauli njema wakiwa nje ya madaraka, wakishika huzidi ubabe, amri na umungu mtu.
 
Tazama hawa wawili waliojinasabisha na ujamaa wakiwa katika mazingira tafauti. Wa kwanza Profesa Mkumbo na wa pili Dr Bashir. Wasomi waliobobea na tuliowaamini mno katika nasaha na fatwa zao wakiwa nje ya uongozi. Walibeba ujamaa, uzalendo na demokrasia tena wakiwa magwiji katika taswira na dira tunayoitaka tena wakizichochea akili zetu katika tafakur nzito na ile ashki ya kudiriki kuota makubwa katika ardhi yetu kuanzia Muungano na Maendeleo ya kiuchumi na katika haki huru.
 
Nakumbuka waraqa wa Profesa Mkumbo wakati akimjibu Mwigulu Nchemba alipomuomba ajiunge nao CCM alipofukuzwa CDM. Akijinata kwa umadhubuti wake wa kusimama na haki huru, usawa, heshima, demokrasia na kuichambua CCM tokea ya Mwalim na waliomfuatia wote kwa nasaba ya msimamo wa haki na demokrasia.

Utaamini kuwa ni yeye leo hii anaethubutu kuwaambia maaskofu wafunge midomo yao hata pale watu wanapouawa kirahisi na kufungashwa katika viroba vya sandarus? Ndie huyu huyu alieitikisa CDM ikabeba itikadi ya ukati na akaisukuma katika ajenda ya haki, demokrasia na uhuru, leo huko aliko yale maandishi yake mwenyewe yanabeba hata robo ya matendo aliokuwa akiyapigania?
 
Ujamaa kama itikadi una mengi mazuri lakini yasiotendeka kwa sababu ya kuenda kinyume na “nature” ya mwanaadam iliojaa ubinafsi, udokozi, ubabe, uonevu na dhana nzima ya nafsi maisha yote kuelemea katika egemezi la ubaya. Utaweza kuyazuia haya kwa kusimamisha haki ilio huru kwa kila mmoja kama binaadam hata awe mzizi mkuu. Haki huru ndio itayosimamisha utu, ubinaadam na kuturejesha katika azma ya ukarimu, ukweli na utulivu wa nafsi inayosimamiwa na uhuru wa haki ili inapokosea ikarekebishika mapema.
 
Kama ilivyo kwa saratani nyengine, tezi dume husababishwa na ukuwaji wa cells ambao hukosa mfumo wa kuzizuia zisiendelee kukuwa. Mpaka sasa haijajulikana hasa sababu ya ukuaji huu usiozuilika lakini kuna theories nyingi zinazobeba dhana ya kuwa genes zinazotumika kuziongoza hizi cells kukua au kuzuia huathirika kiutendaji na matokeo yake ni ukuwaji unaopelekea uvimbe hatari unaoweza kusambaa na kupelekea kifo.
 
maradhi haya humuathiri mwanamme na ishara yake kubwa ni kuenda haja ndogo mara kwa mara ikiwamo pia uwezo mdogo wa kudhibiti haja ndogo. Baadhi ya wakati haja ndogo huambatana na damu, au maumivu makali na halkadhalika uwezo mdogo wa uume kusimama. Lakini katika hatua ya kuenea kwa maradhi haya basi ishara yake kubwa ni maumivu hususan kuanzia kiuno, miguu na uti wa mgongo pamoja na kutoweza kabiza kuzuia haja ndogo na kubwa.
 
Moja kati ya njia za upimwaji wa tezi dume ni kwa hii inayojulikana kama Digital Rectum Examination (DRE). Kwa vile tezi dume yenyewe ipo kwenye ile shingo ya kibofu cha mkojo na haldhalika chini kabisa ya Rectum, njia rahisi ya kupima ni kwa kuingiza kidole kwenye rectum na kuweza kugusa na kuuhisi uvimbe ulipo. Njia hii ni rahisi zaidi na hufanyika hospitalini chini ya uangalizi wa daktari. Anapohisi kuna uwezekano wa uvimbe kuwapo basi hupelekea uchunguzi mwengine wa kitaalamu zaidi.
 
Hapa hutazamwa “biomarkers” yaani viashiria vya chemicals zinazoonekana pale ambapo uvimbe unapoanza kukuwa. Concept ya biomarkers ni kuwa mwili unapoanza maradhi basi ile “Defensive system” huanza kazi ya kuulinda mwili na kuzalisha hizi biomarkers ambazo huwa “specific” kwa kila maradhi. Unapokuta wingi wa biomarkers za prostate huweza pia kutoa ishara ya ukubwa wa maradhi yenyewe pia.
 
mkojo Nao pia unaweza kuonyesha uwepo wa maradhi kwa kutazama PCA3 genes ambazo huonekana kwa cells zile ambazo tayari zimeathirika na tezi dume. Njia hizi ni za gharama mno wakati mwengine hazibebi “value for money” kuliko ile Digital Rectum Examination.
 
#UltrasoundnaBiopsy

Nayo pia hutumika kutoa taswira nzima ya uvimbe, ukubwa wake na kusaidia pia namna hata ya matibabu. Pia upasuaji wa tissue yenyewe katika biopsy kutazama viashiria vya uwepo wa maradhi yenyewe. CT au MRI scan pia hutumika kutazama kama ni ile iliosambaa sehemu nyengine katika mwili na namna ya tiba yake. Mchango wa Dr Humoud ni kuwa ipo “Pelvic ultrasound” ambayo si ghali na inafanyika mara kwa mara.
 
Matibabu yanategemea na hatuwa ya maradhi yenyewe. Katika hatuwa za awali basi upasuaji hutumika katika kuondosha uvimbe wenyewe, au kwa kutumia radiation treatment ambayo mionzi hutumika kwa njia tafauti za kuondoa uvimbe ima kwa radioactive au radiation.

Katika hatua kubwa za ukuaji wa maradhi, basi chemotherapy hutumika kuziua cells za saratani yenyewe moja kwa moja. Vile vile kwa kutazama njia za kupunguza Androgen hormones zinazosababisha kukuwa kwa saratani hii (Androgen Deprivation Treatment ADT) hasa kwa wagonjwa walioathirika na saratani iliokwisha sambaa sehemu nyengine mwilini.

Mchango mwengine wa Dr Hamoud katika topic hii, ni kuwa kwa wale waoga wa upasuaji basi wafahamu mara nyingi matibabu huanza na dawa kwa miezi sita na upasuaji si silaha ya awali ya matibabu bali pale pasipo na budi.
 
Back
Top Bottom