Nakumbuka waraqa wa Profesa Mkumbo wakati akimjibu Mwigulu Nchemba alipomuomba ajiunge nao CCM alipofukuzwa CDM. Akijinata kwa umadhubuti wake wa kusimama na haki huru, usawa, heshima, demokrasia na kuichambua CCM tokea ya Mwalim na waliomfuatia wote kwa nasaba ya msimamo wa haki na demokrasia.
Utaamini kuwa ni yeye leo hii anaethubutu kuwaambia maaskofu wafunge midomo yao hata pale watu wanapouawa kirahisi na kufungashwa katika viroba vya sandarus? Ndie huyu huyu alieitikisa CDM ikabeba itikadi ya ukati na akaisukuma katika ajenda ya haki, demokrasia na uhuru, leo huko aliko yale maandishi yake mwenyewe yanabeba hata robo ya matendo aliokuwa akiyapigania?