Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tunapaswa kuyafikiria madhaifu yetu na dhambi zetu kwa makini sana, kwa kiasi cha kuyashinda madhaifu hayo na dhambi hizo, kabla hatujatoa maamuzi makali dhidi ya wenzetu. Tunawezaje kumlaumu mtu wakati hata sisi wenyewe tunaweza kuwa na matatizo makubwa?
Tusiwe wanafiki. Badala ya kulaumu, saidia.
 
Mfalme Sulemani alikuwa mtu mwenye hekima kuliko wote ulimwenguni. Anatushauri, “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa; Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na BWANA atakupa thawabu (Mithali 25:21-22). Yesu anasema jambo fulani linalofanana sana na hilo katika mafundisho Yake yaliyofuata (Mathayo 5:44-45).
 
Kitendo cha kutukanwa, kupigwa, kushtakiwa au kulazimishwa kubeba mzigo mzito usio wa kwako kinaweza kusababisha mafutu mabaya kabisa katika asili ya binadamu. Yaani, chuki, hasira, ukatili na hata vurugu. Lakini pale wale waliobarikiwa kuwa na hekima wanapojikuta katika majaribu makubwa kama hayo tabia yao haitakiwi kuwa ya shari, inda au ya kulipiza kisasi. Bali inatakiwa kuwa ya kusaidia, kuwa na ridhaa ya kutenda mambo mema, na kuwa mwema kwa wengine siku zote.

mafutu - hisia anazokuwa nazo mtu baada ya kupata maudhi.
 
Kuna kitu kibaya sana ndani ya mtu. Hilo liko wazi. vitbu vya dini vinasema chanzo cha matatizo ya mtu ni moyo wake, roho yake, pamoja na uwezo wake wa kufikiri. Tumejaa ulaghai, unafiki na utata. Tunajichezea sisi wenyewe ule mchezo wa kitoto wa kombolela. Yaani, tunajificha na kujitafuta wenyewe, tunawadanganya watu lakini Mungu anatuona.
 
Shetani na wafuasi wake wako kifungoni sasa hivi kwa sababu dhambi walizotenda hazisameheki. Dhambi ya kumkana Mungu na kumkubali Shetani haisameheki. Kwa maneno mengine, ukimuuzia Shetani roho yako, jina lako halitaandikwa katika kitabu cha uzima litaandikwa katika kitabu cha mauti. Kama itakubidi kuuza roho, usimuuzie Shetani
 
Afrika imekaliwa na mizimu. Wazungu hawataweza kumaliza mali ya Afrika. Mali ya Afrika ni ya Waafrika wenyewe. Itamalizwa na sisi wenyewe.

Afrika isomeshe watu wake, na itumie vizuri mapato yanayotokana na mauzo ya rasilimali zake kwa faida ya jumla ya wananchi wa nchi zake, kusudi baadaye wawe wataalamu wa rasilimali za nchi zao wenyewe, kuepukana na utumwa wa rasilimali. Rasilimali za Afrika zina miiko na masharti yake.
 
Mwaka mpya ukifika watu husherehekea kwa vifijo na nderemo! Pumzi ikifika hawasherehekei. Kwa nini?

Kitu cha kwanza kufanyika mwanadamu anapozaliwa ni kuvuta pumzi ya kwanza katika mapafu ya mwili wake. Cha mwisho kufanyika kabla ya kufa ni kutoa pumzi ya mwisho katika mapafu ya mwili wake. Pumzi iliyoingia kwanza baada ya kuzaliwa, itakuwa ya mwisho kutoka kabla ya kufa.
 
Pumzi ni bora kuliko muda halafu pumzi ni uhai. Bila uhai watu hawataweza kusherehekea mwaka mpya au kufanya chochote. Likumbuke jina la Mwenyezi Mungu katika kila pumzi unayoingiza na kutoa.

Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya mtu baada ya mtu kufariki? Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya pumzi katika kipindi ambacho mtu hana uwezo tena wa kuvuta hewa? Nini thamani ya pumzi? Thamani ya pumzi ni kukufanya uwe wewe na si udongo.
 
Unachagua sentensi fupi au maneno rahisi kuhusu Mungu unayoweza kuyasema na kuyarudia kimoyomoyo kila siku katika kila pumzi inayoingia na kutoka ndani ya mapafu yako! Kwa mfano: “Asante Mungu.” “U pamoja nami.” “Nataka kukujua.” “Napokea neema yako.” “Nakutegemea wewe.” “Mimi ni wako.” “Nisaidie nikuamini.” “U Mungu wangu.” “Naishi kwa ajili yako.” “Nisamehe dhambi zangu zote.”

Fundisha akili yako kumkumbuka Mungu kila wakati.
 
Lakini Shetani atakapoinasa roho hiyo, kabla mwenye nayo hajazaliwa, ataibadilisha ili izaliwe sehemu nyingine tofauti na pale alipopanga Mungu; ili imtumikie yeye badala ya kumtumikia Mungu.

Kujua uraia halisi wa roho yako, hivyo kuujua uraia wako, lazima ujitambue; lazima ujue kwa nini ulizaliwa.
 
Kiburi ni kiwango cha juu kabisa cha umimi au ubinafsi, na ni sumu ya mahusiano.

Kuwa na kiasi. Usiwe mjinga sana wala usiwe mjanja sana. Ukiwa mjinga sana utapata matatizo, kwa Mungu na kwa wanadamu, na ukiwa mjanja sana utapata matatizo pia, ambayo ni kiburi, kwa sababu mtu mwenye kiburi hawezi kamwe kuridhika na heshima na unyenyekevu anaoupata kutoka kwa watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…