Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Watu wenye kiburi ni wabinafsi, watu wanaopenda kuheshimiwa na kunyenyekewa, na wanajiona bora zaidi kuliko wengine, wanaopata taabu sana kuomba msamaha. Kiburi si upendo na upendo si kiburi. Dawa ya kiburi si kiburi kingine. Dawa ya kiburi ni upendo na hekima.

Hata hivyo, kuna tofauti kati ya kutokujiamini na kiburi. Mtu anaweza asijiamini na asiwe na kiburi, na anaweza asijiamini na akawa na kiburi.

Wengine wanasema kiburi ni kizuri, kwamba ili umshinde Shetani lazima uwe na kiburi. Lakini kiburi dhidi ya Shetani unakishinda kwa hekima.
 
Shetani na wafuasi wake wako kifungoni sasa hivi kwa sababu dhambi walizotenda hazisameheki. Dhambi ya kumkana Mungu na kumkubali Shetani haisameheki. Kwa maneno mengine, ukimuuzia Shetani roho yako, jina lako halitaandikwa katika kitabu cha uzima litaandikwa katika kitabu cha mauti. Kama itakubidi kuuza roho, usimuuzie Shetani
Mambo haya yanatisha. Wengine wanakuambia eti ile kutenda dhambi huku ukijua kuwa ni dhambi ( mf. Kumnyandua demu ambaye siyo mke wako) tayari ni kumkufuru Roho Mtakatifu na kujikabidhi rasmi kwa shetani...na kwamba dhambi hiyo haisameheki. Nani atakwenda mbinguni sasa?
 
Mambo haya yanatisha. Wengine wanakuambia eti ile kutenda dhambi huku ukijua kuwa ni dhambi ( mf. Kumnyandua demu ambaye asiye mke wako) tayari ni kumkufuru Roho Mtakatifu na kujikabidhi rasmi kwa shetani...na kwamba dhambi hiyo haisameheki. Nani atakwenda mbinguni sasa?
Mkuu mambo ya imani yapo shaghalabaghla.
naamini Mungu anasamehe pindi unapoelekea kwake kuomba msamaha.
baadhi ya wanazuoni wanamtafsiri Mungu kama ni mwenye sifa za mwanadamu kwa kujawa na sifa za ukatili mkubwa sana kwa viumbe wake na asiyefahamu msamiati wa kuomba msamaha
 
Sababu kubwa inayofanya mwanamke au mwanamume ajishauri kumkubali mwanamume au mwanamke badala ya kujishauri kumkataa ni nguvu ya uchumi aliyonayo mwanamume au mwanamke anayetongoza. Kumkataa mtu mwenye nguvu ya uchumi ni vigumu sana hata awe mbaya kiasi gani. Maana nguvu ya uchumi haiangalii sura wala umbile la mtu.
 
Mwanamke anayejishauri kumkubali mwanamume yeyote mzuri au mwenye pesa, au mbaya na mwenye pesa, au mzuri na mwenye pesa, ni kibiritingoma. Yule anayejishauri kukataa ni muungwana.

Mwanamume anayejishauri kumkataa mwanamke yeyote mzuri au mwenye pesa, au mbaya na mwenye pesa, au mzuri na mwenye pesa, ni muungwana. Yule anayejishauri kukubali ni kibiritingoma.
 
Kiungo cha binadamu kinachofanya watu waongezeke hatukupewa ili tukitumie kwa anasa za ulimwengu huu. Tulipewa kwa ajili ya kuongezeka tukiwa katika taasisi rasmi ya ndoa, kama upendo wa Mungu

Mungu alipomuumba Adamu na Hawa amri ya kwanza aliyowapa ni kufanya mapenzi, ili waijaze dunia, wakiwa katika taasisi ya ndoa. Hivyo, mapenzi nje ya taasisi ya ndoa ni dhambi inayostahili aibu.
 
Kitu kigumu kuliko vyote usikikatie tamaa, hasa kile unachojua kikifanikiwa kitasaidia watu wengi, kwani kuna uwezekano kikawa kizuri na chenye manufaa zaidi kuliko vyote.

Unapokuwa unafukuzia ndoto, njia ya kuifikia ndoto hiyo aghalabu huwa ngumu sana; lakini pale inapotimia, ndoto hiyo huwa kitu kizuri kuliko vyote.

Kama kwako msamaha ni kitu kigumu kuliko vyote ni kizuri kuliko vyote ukiumudu, kwani kigumu kuliko vyote ni kizuri kuliko vyote.
 
Mkuu mambo ya imani yapo shaghalabaghla.
naamini Mungu anasamehe pindi unapoelekea kwake kuomba msamaha.
baadhi ya wanazuoni wanamtafsiri Mungu kama ni mwenye sifa za mwanadamu kwa kujawa na sifa za ukatili mkubwa sana kwa viumbe wake na asiyefahamu msamiati wa kuomba msamaha

Yeye ni mwingi wa Rehema japo kuna baadhi ya watumishi ukiwasikiliza unaweza hata kujikatia tamaa tu. Asante kwa angalizo hili...
 
Mbinguni, Shetani alikuwa kiongozi wa kwaya. Duniani, anatumia muziki kuteka dunia.

Shetani alikuwa mtaalamu wa muziki huko mbinguni. Hakuna aliyekuwa akiimba kama yeye. Huku duniani anatumia utaalamu huo kuteka dunia nzima. Anatumia muziki wa kidunia na muziki wa injili, kusudi binadamu asiende mbinguni.
 
Mwimbaji anaweza kuwa na nia njema kabisa na muziki wake; lakini Shetani akautumia muziki huo kwa siri, hata kama ni muziki wa injili, kusambaza dhambi ulimwenguni kote.

Si rahisi kumshinda Shetani. Kumbuka, amekuwepo hapa kwa zaidi ya miaka 6000. Sisi hata miaka 300 hatujafikisha. Yaani, hakuna mtu mwenye umri wa miaka 300 hapa duniani leo. Anatujua kiasi gani? Anatujua sana.
 
Kwa nini Range Rover ina viti zaidi ya vitano? Ili dereva asisafiri peke yake. Ukiona umefanikiwa sana au umeshindwa sana katika maisha, ujue kuna kitu Mungu anataka kutoka kwako kwa ajili ya wengine.

Mungu anataka tusaidiane na tushukuru kwa kila jambo kwani yeye ndiye aliyetuumba, na anajua kila kitu kuhusu maisha yetu.

Katika barabara ya mafanikio, usisafiri peke yako, safiri na wenzako.
 
Tajiri anaweza kupita na gari lake katika kituo cha daladala wakati mvua ikinyesha, na akaona si vizuri kuchukua hata watu wawili akawapa lifti, licha ya kuwa gari lake linaweza kuwa na nafasi ya watu sita! Katika dunia hii ambapo dereva na abiria wote wanaweza kuwa hatari, hilo linaweza kuwa jambo lisilowezekana. Lakini kiroho, huo ni ubinafsi na Mungu hapendi.
 
Kiungo cha binadamu kinachofanya watu waongezeke hatukupewa ili tukitumie kwa anasa za ulimwengu huu. Tulipewa kwa ajili ya kuongezeka tukiwa katika taasisi rasmi ya ndoa, kama upendo wa Mungu

Mungu alipomuumba Adamu na Hawa amri ya kwanza aliyowapa ni kufanya mapenzi, ili waijaze dunia, wakiwa katika taasisi ya ndoa. Hivyo, mapenzi nje ya taasisi ya ndoa ni dhambi inayostahili aibu.
Dhambi hii itaangamiza wengi. Na ile ya kutamani tamani. Na kusema uwongo...Mungu na Atusaidie kwa sababu hakuna namna...
 
Wema usizidi uwezo ni falsafa ya kidunia, haina maana. Wema hauozi ni falsafa ya Kimungu, ina maana.

Kufanikiwa katika maisha kuna changamoto zake na kushindwa katika maisha kuna changamoto zake pia. Lakini maskini ana changamoto nyingi kuliko tajiri. Tajiri msaidie maskini na maskini msaidie tajiri.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]. Wabongo maneno mengi mno jamani !!!
IMG-20190523-WA0058.jpeg
 
Back
Top Bottom