Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Aisee. Wenye hela nao kumbe wanapataga shida?
 
Kwenye Ligi Kuu tano bora za huko Ulaya, Paris Saint-Germain ya Ligue 1 imefunika timu nyingine kutoka kwenye ligi hizo tano kutokana na kuwa na fowadi matata kwenye kufunga mabao. Katika ligi ya msimu huu, timu hiyo imefunga mabao 105, ikizizidi timu kama Manchester City iliyofunga mabaoa 95 kwenye Ligi Kuu England, Barcelona mabao 90 kwenye La Liga na Bayern Munich mabao 88 kwenye Bundesliga.
 
Messi alifunga mabao 36 katika mechi 34 alizocheza La Liga msimu huu na hivyo kushinda Kiatu cha Dhahabu cha ligi za Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo, mara saba katika historia yake kwenye soka. Mpinzani wake, Cristiano Ronaldo yeye aliwahi kushinda mara mbili mfululizo kiatu hicho cha Ulaya.
 
Juve wagawa dozi mfululizo

Mabingwa wa soka wa Serie A, Juventus iliweka rekodi ya kushinda mechi 27 mfululizo katika msimu wa 2018/19, ikiwa mechi nyingi zaidi kuwahi kufikiwa na klabu zote 98 zilizocheza kwenye Ligi Kuu tano bora za huko Ulaya.
 
Kiwango hicho walichoonyesha kwenye Ligi Kuu England, ikiwa ni idadi ndogo ya mabao kuliko timu nyingine yoyote kwenye ligi hizo tano bora Ulaya. Lille wao kwenye Ligue 1 wamefunga mabao 33, Atletico Madrid kwenye La Liga mabao 29 na RB Leipzig kwenye Bundesliga imeruhusu mabao 29.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…