Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

hapana shaka mzee mwenye zaidi ya umri wa miaka 50, akisoma majina ya Jim Reeves, atakuwa umeguswa vilivyo. Jim Reeves alikuwa mwanamuziki toka nchini Marekani, aliyekuwa amejikita katika miondoko ya muziki wa ‘Country’ na muziki wa kawaida akiwa mtunzi halikadhalika uimbaji.
 
Katika maisha yake ya muziki, aliweza kuweka rekodi ya kuupandisha ‘chati’ muziki wake kati ya miaka ya 1950 hadi ya 1980. Nyimbo za Jim Reeves husikika sana katika baaadhi ya sherehe zinazowajumuisha wazee hususani katika mikoa ya Nyanda za Kaskazini, nyakati za sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.
 
Reeves alipata kuwa maarufu na akajulikana kama mwanamuziki wa midundo ya ‘Nashville’ (ambayo ni mchanganyiko wa muziki wa zamani wa Country na ule wa kisasa). Wasifu wa nguli huyo unaonesha kuwa majina lake halisi alikuwa ikiitwa James Travis aka “Jim”.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…