Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza’ Usemi huu ulijidhihirisha kwa Mapangala baada ya kuonyesha umahiri mkubwa kupitia sauti yake nyororo kulipelekea kupata kazi ya kupiga muziki kwenye bendi za Bariza, Super Tukina, Bella Bella na Saka Saka katika jiji la Kinsahasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
 
Ili kuonyesha ukomavu katika muziki, Samba aliamua kujitegemea mwenyewe kwa kuunda bendi yake na kuipa jina la Orchestra Virunga mwaka 1981 bendi ambayo kwa kipindi kifupi ikakubalika na wapenzi wa muziki na kuwa moja kati ya bendi maarufu Afrika Mashariki.
 
Samba Mapangala hupiga muziki wake ukiwa na mchanganyiko wa staili za rumba na Soukous kutoka Kongo. Ili kuwaridhisha wapenzi wa muziki wa Nairobi na vitongoji vyake walipiga muziki kwa staili za watu wa Kenya. Rekodi ya kwanza ya Virunga iliyoitwa ‘It's Disco Time with’ ilitoka mwaka 1982.
 
Hahaha
 
Mapangala na bendi yake ya Virunga walisafiri kwenda nchini Uingereza mwezi Aprili 1991 na huko walifanya maonyesho makubwa takribani 23. Baada ya kufurahia mafanikio ya safari yao, walifanya safari nyingine ya mwisho mwaka 1997 wakipitia nchi za Afrika hadi Marekani ya Kaskazini.
 
Album za Samba Mapangala zilizopo ni pamoja na Virunga Volcano ya mwaka 1990, Evasion ya 1983, Feet on Fireya ya 1991, na Karibu Kenya iliyofyatuliwa mwaka 1995 zilizorekodiwa katika jiji la Paris nchini Ufaransa akiwashirikishwa wanamuziki toka bendi ya Les Quarters Etoiles na wanamuziki wengine nguli waliokuwa hapo Paris.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…