Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nimetengeneza app kwa ajili ya PDF Files inaitwa All PDF inapatikana play store

All PDF android app

* Read PDF Files
* Merge multiple PDF files into a single file
* Split a PDF file into multiple Files
* Extract images from a PDF file
* Save PDF pages as images
* Share PDF file as image
* Compress PDF file to reduce file size
* Edit PDF metadata like title, author, creator etc.

The app is available on Google play store at https://play.google.com/store/apps/details?id=tz.co.wadau.allpdf
 
hongera sana mkuu.
 
MWANI THERESA NTARE- MALKIA WA WAHA NA CHIFU MWANAMKE WA KASULU.

Francis Daudi, Vijayanagar!

Ni wanawake wachache tu wanapatikana katika kurasa muhimu za Historia ya Tanzania. Nimepata kuandika historia ya Bibi Titi Mohamed, Binti Namabengo na Mkomanile au Nkomanile(Mwanamke shujaa wa Vita vya Majimaji).
Leo ninawaletea historia ya mwanamke shupavu ambaye alikuwa ni mtawala wa kutoka katika kabila la Waha wa jamii ya kitutsi, ukanda wa Kasulu sehemu za Heru Juu. Huyu ni Mwami Theresa Ntare VI, Malkia wa Heru kuanzia 16 Aprili, 1946 mpaka 9 Novemba, 1962.
 
Unapajua Heru?

Heru ni eneo ambalo lipo katika wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma. Eneo la Heru limegawanyika katika sehemu mbili (Heru juu na Heru chini). Heru Chini inaundwa na vijiji vya Nyansha, Mgandazi, Ntare, Bugaga, Nyumbigwa, Nkundutsi, Zeze na vijiji vyote vya maeneo ya Kasulu ya chini. Heru juu inaundwa na vijiji vya Munyegera,Heru na Buha pamoja na vijiji vya ukanda wote wa juu kuelekea Buhigwe.
 
Kihistoria Wanyaheru (Buha) ndio hasa Waha asilia na Kiha cha Heru (Buha) kina tofauti ya kimatamshi na jamii zingine za Waha. NGOMA ZA BWAMI ambazo ni maarufu kwenye kabila la Waha zinaelezwa kushamiri eneo la Heru zaidi kuliko maeneo mengine.

Mengi hayajulikani katika historia ya utoto wa Mwami Theresa Ntare, lakini inaaminika alikuwa mtoto wa kike pekee wa Chifu Ntare. Inaelezwa kwamba Mwami Thereza Ntare alitawazwa uchifu baada baba yake Mwami Ntare kukosa mtoto wa kiume. Baada kutawazwa uchifu ilibidi atafutiwe mchumba kutoka ukoo wa Chifu Lusimbi wa Kalinzi hivyo akawa ameolewa na kijana wa kitutsi kutoka Kalinzi akiitwa Bw. George Shinganya.
 
Kulingana na mila za Kiha, Mwami haolewi. Akiolewa inabidi ahame milki yake ya Uchifu ili akawe mke wa huyo muoaji. Hivyo basi, Mwami Ntare hakuolewa na Bw. George Shinganya. Bali familia ya Mwami ndiyo iliyolipa mahari kwa familia ya Bw. George Shinganya. Hivyo, Jina la Shinganya likaondolewa na akaitwa George Ntare.

Baadaye ndoa ya Mwami Theresa Ntare na George ilivunjika na Mwami Theresa Ntare akaoana na Mwami Louis Dantes Ngua wa Ufipa(Huyu ana asili ya uchifu wa Ufipa). Kuna nadharia zinazoeleza pia kuwa Mwami Theresa Ntare alipata pia kuwa mke wa Chifu Makwaia wa Usukuma. Lakini hakuna ushahidi wowote juu ya hilo.
 
Wakati wa zama hizo jamii nyingi za Kiafrika zilitajwa kuwaweka nyuma wanawake hasa katika masuala ya Uongozi. Hilo halikumfanya Mwanamama Mwami Theresa Ntare asiweze kuongoza vizuri na kishupavu jamii yake ya Waha wa Heru huko Kasulu.

Hakuishia hapo, mama huyu aliweza kushika wadhifa mkubwa ambapo alikuwa ni Mkuu wa machifu wote Tanganyika akipokea kijiti kutoka kwa Chifu Petro Itosi Marealle mwaka 1958. Makabidhiano yalifanyika shule ya sekondari ya Mzumbe, na mpaka sasa Mzumbe kuna bweni linaitwa Ntare.
 
Mwani Theresa Ntare aliheshimika kama chifu wa Kasulu yote na sio tu Heru alisimamia vyema msimamo wa Baraza la Machifu mwaka 1958 na kuunga mkono juhudi za TANU katika kudai uhuru.

Mwami Theresa Ntare alikuwa ni mmoja ya Wabunge wachache wa Baraza la Kutunga Sheria la Tanganyika kabla hata ya Uhuru wa Tanganyika
 
Aliendelea kuwa Mbunge mpaka miaka ya 1980, lakini kabla ya hapo aliachia uchifu Disemba 9, 1962, Katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam nchini Tanganyika. Hapo alikaribishwa kama Malkia wa Heru kwa Ngoma Maalumu kutoka Ngome ya Malkia wa Heru kwa heshima kubwa.

Inaelezwa alifariki miaka ya 1990 na mara ya mwisho alikuwa akiishi maeneo ya karibu na barabara inayoelekea Munyegera - Kati ya ilipo shule ya msingi na Kahaga Dispensary (kulikuwa na soko hapo kati miaka ya 1985).
 
Kwa sasa Mwami wa Heru ni sasa Costa Shinganya au Ntare ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mwani Theresa Ntare.

Kuna wanaosema Mbunge wa Kigoma mjini, ndugu Zitto Ruyagwa Kabwe ndiye hasa Mwami wa Waha wote. Lakini hili ieleweke yeye amepewa heshima tu ya Mwami Mpole aliyejulikana kama Ruyagwa.

Huyu ndiye Mwami Theresa Ntare VI, Malkia wa Heru kuanzia 16 Aprili, 1946 mpaka 9 Novemba, 1962.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…