Kikosi hicho cha Etihad kinachonolewa na Mhispaniola, Pep Guardiola kilijivunia kuwa na safu moto ya washambuliaji watatu iliyoundwa na Sergio Aguero, Raheem Sterling na Leroy Sane, ambao wamehusika kwenye mabao 48 kwenye ligi. Safu hiyo ya kombinesheni ya fowadi watatu, Aguero amefunga mabaoa 21, Sterling ameweka wavuni mara 17 na Sane amefunga mara 10.
Fowadi hiyo ndiyo iliyoibeba Man City na kutamba kwenye Ligi Kuu England ikibeba ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo. Sane anahusishwa na mpango wa kuondoka kwenye timu hiyo ambapo Bayern Munich inapiga hesabu za kuinasa saini yake