Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ARSENAL imeshasikia chokochoko za mastaa wake Alexandre Lacazette na Pierre-Emerick Aubameyang kuwindwa na timu nyingine, hivyo wameanza mchakato mapema wa kusaka mtu wa kuja kuziba pengo lao na mabao yakaendelea kupatikana.
 
Kikosi hicho cha kocha Unai Emery kimeanzisha mpango wa kwenda kumsajili staa wa CSKA Moscow, Fedor Chalov, ambaye ni kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu Russia, ambaye anasakwa pia na vigogo Monaco na Sevilla.
 
Kocha Emery anajaribu kusaka wachezaji wakali kwa kuzingatia bajeti yake ya Pauni 40 milioni, licha ya kwamba anaamini ataingiza mkwanja mrefu zaidi kama mastraika wake matata Aubameyang na Lacazette wataamua kuondoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…