Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Liverpool ni timu kubwa ya soka na wamethibitisha ubora wao kwa kurudi tena katika fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya pili mfululizo, lakini wachezaji wengi wanapata shida kusema hapana pindi Real Madrid na Barcelona zinapowafuata.”
 
Tuliona hapo nyuma kwa Luis Suarez na Philippe Coutinho. Ingawa walikuwa wanafurahia kucheza soka Liverpool, lakini mawazo yao yalibadilika pindi walipotakiwa na Barcelona. Hilo litatokea tena kwa Mane na Salah,” aliongeza Souness.
 
Hata hivyo, Souness alikiri kwamba kwa sasa Liverpool wapo katika nafasi nzuri baada ya kutwaa taji la sita la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya Jumamosi iliyopita baada ya kuichapa Tottenham mabao 2-0 katika dimba la Wanda Metropolitano jijini Madrid.
 
Lakini anaamini kwamba Liverpool inabidi iwe na wasiwasi zaidi kuhusu wachezaji wanaoweza kuondoka kuliko wale wanaoweza kuingia huku pia akiwa na wasiwasi na nguvu ya matumizi ya pesa kutoka kwa wapinzani wao wakubwa katika Ligi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…