Na moja ya sababu kubwa ya wengi wetu kushindwa kufikia kilele cha mafanikio hayo ni kwamba tumeshindwa mbinu madhubuti ya kukusanya vipande hivyo na kuviweka pamoja ili tuweze kufankiwa.
Leo nitakueleza ni kipande ambacho ni muhimu unachopaswa kukiunganisha katika maisha yako ili uweze kufanikiwa kiurahisi, Kwani wengi wa watu ambao wameweza kufanikiwa katika sayari hii ni kwamba waliweza kufanikiwa kipande hiki hatimaye kuweza kufanikiwa.
Kipande hicho si kingine bali ni unahitaji mtandao wa watu ili uweze kufanikiwa. Moja kati ya changamoto kubwa ambayo ipo na inaendelea kutuuua taratibu ni kwamba hatuna watu sahihi ambao wanasabisha sisi kuweza kusonga mbele katika harakati za kufanikiwa.
Wengi wetu, Watu tulionao ni wale wale wa siku zote ambao ukiwambia unataka kufanya jambo Fulani lenye tija ni lazima watu hao watakuleleta sababau za kushindwa tu. Watu wa aina hii hawafai hata chembe na vyema kuwaepuka mapema.
Hebu fanya zoezi dogo shika simu yako kisha pekua majina ya watu mbalimbali waliopo katika simu yako, je majina mangapi yana manufaa/msaada kwako? Jibu baki nalo.
Nimukuuliza swali hili kwa sababu asilimia 99.999 wengi wetu simu zetu zimejaa majina ambayo hayana chachu yeyote katika kuhakikisha tunapiga hatu za kimafankio.
Nini kifanyike; Ukiona simu yako haina majina matano ambayo yanachangia kitu chochote kwenye maisha yako basi simu hiyo iweke kwenye maji kwani haina umuhimu wowote kwako (hapa nimetia chumvi).
Ila ukweli ni huu, Unachotakiwa kufanya ni kwamba katika maisha yako ya kila siku hakikisha ya kwamba unazungukwa na watu chanya wenye kuchangia jambo fulani katika maishha yako ya kila siku.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.