Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sasa wakati hapa kwetu Tanzania idadi ya wanaume ndio ndogo kulinganisha na wanawake, kwa nchi za wenzetu mambo ni tofauti kabisa, na idadi ya wanawake ni robo ya wanaume wote kwenye nchi hizo ambapo asilimia 72% ndio wanaume na asilimia 28% ndio wanawake.
 
Kwa mfano huo, Na kwa sababu hizo basi, tofauti na ilivyo kwa Tanzania mabinti wakikosa wanaume waku-waoa, hii hapa orodha nyingine kabisa ya baadhi ya (Nchi-12) zinazoongoza duniani kwa kuwa na upungufu wa wanawake na sio Wanaume kiasi kwamba pindi mtoto anapozaliwa huwekewa (oder) na wazazi wenye mtoto wa kiume kwa minajili ya kuchukua jiko katika nyumba hiyo kwa siku za baadaye pindi watoto wao watakapokua kwa kuwa Vijana wao wanakabiliwa na tatizo la kukosa au kuwa na wakati mgumu kupata wenzi wao wa maisha.
 
Qatar





Nchi ya Qatar iliyopo katika nchi za kiarabu ni miongoni wa nchi ambazo kuna upungufu wa mabinti, na kushikilia rekodi hiyo kwa muda mrefu kwa sasa. Sababu kubwa ya upungufu huo ni pamoja na taratibu na sheria ya nchi hiyo inayozingatia maadili ya kiislamu zaidi na hivyo kutopendelewa zaidi na mabinti na raia wengine kuingia nchini humo, ikichagizwa na serikali ya nchi hiyo kutotoa visa kwa (Jinsia ya kike) wa mataifa wengine ispokuwa Uingereza na Canada pekee.
 
61687902_180361759642398_6836092314105922081_n.jpg
 
Sababu nyingine kubwa ni uzalianaji duni, tokea pale wanaume (karibu-94%) huihama nchi yao na kwenda kufanya kazi mataifa mengine ya kigeni kiasi ya kwamba serikali ya Qatar kwa sasa ikawalazimu kutoa nafasi za wahamiaji na kuwapatia kibali maalumu (Visa) ili kuziba upungufu huo wa nguvukazi taifa waliohama makwao kwa ajili ya kutaka kuinua uchumi wan chi hiyo.

Uwiano (ratio) kati ya wanaume na wanawake kwa nchi hii iliyo mashariki ya kati na iliyo tajiri kwa uzalishaji wa mafuta ni 3.41 to – 1.54.
 
United Arab Emirates (UAE)





Hadi kufikia karne ya (20th-century), UAE ilikuwa na upungufu wa karibu watu 40,000 kwa raia wazawa, huku wanawake pekee wakiwa 22,000, hiyo ikitokana na raia wake kuhama nchi hiyo na kwenda nchi jirani kutafuta maisha kabla ya kugundulika kwa mafuta, ambapo kidogo kwasasa idadi ya wakazi wake imeongezeka kidogo, huku wengi (85%) wakiwa sio raia wa nchi hiyo bali wapo hapo kula maisha. Wengi mtakubaliana na mimi kwa kufanya utafiti mdogo tu wa wakaazi wa dubai, kwa kuangalia wazawa na wale wasio wazawa.
 
Lakini katika kuongezeka huko bado uwiano baina ya wanaume na wanawake sio sawa, ambapo kwasasa inawalazimu wanaume wan chi hiyo kwenda nchi nyingine za kiarabu kutafuta wachumba huko.

UAE pato lake kubwa hutokana na Mafuta na Utalii, kwa wageni kutoka mataifa mbalimbali kwenda nchini humo kula bata.
 
India



India inashika nafasi ya 3 kuwa na upungufu wa mabinti duniani, ingawa tunaweza kusema inashika nafasi ya3 duniani kwasasa kwakuwa na watu wengi ukiacha China na Marekani, huku idadi ya raia wake ikikisiwa kuzipita China na USA na kushika nafasi ya kwanza ifikapo mwaka2024. lakini wengi wa watu hao bado wanaume ndio wengi.
 
Uwiano uliopo kwasasa kati ya wanaume na wanawake nchini humo ni asilimia karibu 1.08 ya kila mwanaume kwa mwanamke mmoja, yaani sawa na tuseme kila mwanamke wa india awe na wanaume 5 kuleta uwiano sawa.
 
Ukilinganisha na nchi za (G-20) na ikiwa miongoni, India kwasasa inapiga hatua kimaendeleo zaidi duniani ingawa bado kuna changamoto za wanandugu kuendelea kushikamana pamoja, wazee wakiwa wengi kuliko nguvu kazi ambapo ni vijana na hivo wanaume wenye uwezo kidogo kuwasaidia wazazi na ndugu zake wote.
 
Sababu kubwa ya upungufu huo haijawekwa bayana lakini watafiti wanaamini kuwa Wanaume wa nchi hiyo huwa na bahati sana ya kupata watoto wa kiume kuliko wa kike, hivyo familia moja yenye watoto 7, wakike ni wawili tu pekee
 
Back
Top Bottom