Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

9. Yaya na Kolo Toure - Euro 48.7 milioni

Ndugu wawili, Yaya na Kolo Toure wote walipata mafanikio makubwa kwenye soka lao. Kaka mkubwa, Kolo alipata mafanikio akiwa na Arsenal, wakati mdogo mtu, Yaya alikuwa moto kabisa huko Barcelona. Ndugu hao wote walihamia Manchester City, ambako Yaya alitengeneza jina kubwa zaidi. Lakini, Man City iliponasa huduma zao kwa ujumla ililipa kiasi cha Euro 48.7 milioni na kufanya ndugu hao kuwa miongoni mwa waliozigharimu timu pesa nyingi.
 
Alikwenda kubeba mataji kibao huko Old Trafford ikiwamo Ligi ya Mabingwa Ulaya. Rio alikuwa na ndugu yake, Anton Ferdinand, ambaye pia alikuwa akicheza beki, ambapo kuna wakati aliigharimu Sunderland Euro 10 milioni kupata saini yake. Kwa ujumla ndugu hao wakazigharimu timu Euro 56 milioni.
 
7. Anthony na Johan Martial - Euro 60.8 milioni

Anthony Martial alifanya uhamisho wa kibabe alipotua Manchester United kutoka Monaco kwa dili lililokuwa la Euro 60 milioni. Hayo ndiyo makubaliano yaliyokuwa yamefikia kwenye dili hilo la Martial kutua Old Trafford. Kaka yake mkubwa, Johan Martial, naye ni mwanasoka na wakati ananaswa na Stade Brest 29 timu hiyo iliipa SC Bastia Euro 800,000 kupata huduma yake na hivyo kufanya kwa ujumla wake ndugu hao kugharimu Euro 60.8 milioni.
 
6. Kaka na Digao - Euro 67.5 milioni

Kaka alikuwa mmoja kati ya wanasoka mastaa kabisa duniani hasa kutokana na soka lake matata alilocheza AC Milan. Mbrazili huyo alishinda Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Brazil. Real Madrid ililipa Euro 67 milioni kuinasa huduma yake mwaka 2009 kutoka AC Milan.
 
5. Romelu na Jordan Lukaku - Euro 88.7 milioni

Man United ilimnasa Romelu Lukaku kwa Euro 84.7 milioni. Mdogo wake anacheza huko Lazio, ambayo ilimsajili kutoka KV Oostende kwa ada ya Euro 4 milioni. Ukijumlisha ada zote zilizolipwa kwa ndugu hao utaona wamezigharimu timu Euro 88.7 milioni.
 
5. Romelu na Jordan Lukaku - Euro 88.7 milioni

Man United ilimnasa Romelu Lukaku kwa Euro 84.7 milioni. Mdogo wake anacheza huko Lazio, ambayo ilimsajili kutoka KV Oostende kwa ada ya Euro 4 milioni. Ukijumlisha ada zote zilizolipwa kwa ndugu hao utaona wamezigharimu timu Euro 88.7 milioni.
 
4. Gonzalo na Federico Higuain - Euro 91.3 milioni

Gonzalo Higuain amekumbana na nyakati ngumu katika maisha yake ya soka kwa siku za karibunni, hasa katika kipindi hiki alichokuwa Chelsea, mambo hayakuwa mazuri kabisa. Lakini wakati akitoka Napoli kwenda Juventus huduma yake iligharimu Euro 90 milioni.
 
3. Lucas na Theo Hernandez - Euro 104 milioni

Lucas Hernandez aliibukia kwenye timu ya watoto ya Atletico Madrid na kutamba kwenye kikosi cha wakubwa kwa haraka sana. Mfaransa huyo alitamba kwa miaka minne katika kikosi cha Atletico kabla ya kuuzwa kwenda Bayern Munich kwa ada ya Euro 80 milioni. Ndugu yake, Theo Hernandez naye aliuzwa na Atletico kwenda Real Madrid kwa Euro 24 milioni na kufanya ndugu hao wawili huduma yao kugharimu Euro 104 milioni.
 
Wakati huo, ndugu yake, Florentin Pogba, naye aliigharimu Saint-Etienne kiasi cha Euro 500,000, wakati ilipomsajili kutoka CS Sedan na hivyo kufanya huduma za ndugu hao wawili kuzigharimu Euro 105.5 milioni na kuwa moja ya ndugu walionaswa kwa pesa nyingi katika historia ya mchezo huo wa soka duniani.
 
1. Eden na Thorgan Hazard - Euro 125.5 milioni

Eden Hazard ametua Real Madrid hivi karibuni akitokea Chelsea na imedaiwa wababe hao wa Bernabeu wameshalipa Euro 100 milioni na nyingine zitalipwa baadaye baada ya msimu kuanza.
 
Lakini kwenye dirisha hili hili la majira ya kiangazi, Borussia Dortmund nayo ililipa Euro 25.5 milioni huko Borussia Monchengladbach kunasa huduma ya winga Thorgan na hivyo kufanya ndugu hao wawili, Eden na Thorgan uhamisho wao kuwa Euro 125 milioni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…