Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Timu Messi leo wako wapi? Cole Williams na King Davet njooni huku GOAT wenu anasemwa [emoji16][emoji16][emoji16]

Na Prisca njoo uchukue points zaidi za kuwa unatumia kumtetea CR7 wako [emoji16][emoji16][emoji16]
 
TAHARUKI ilizuka siku ya jana Ijumaa baada ya msafara wa timu ya taifa ya Cameroon kushindwa kuwasili nchini Misri tayari kwa kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) kama ilivyotegemewa kutokana na mgomo ulioanzishwa na wachezaji wa timu hiyo kabla hawajaondoka nchini mwao kutokana sababu mbalimbali.
 
Sababu kuu ambayo iliwasukuma nyota hao kugoma hadi kufikia hatua Kocha Mkuu, Clarence Seedorf kumuomba nyota wa zamani wa Cameroon kuitatua ilikuwa ni madai ya stahiki za bonasi kwa wachezaji ambazo walipaswa kulipa kwa kufuzu AFCON.
 
Inadaiwa kuwa Shirikisho la Soka Cameroon (FECAFOOT) limewapa bonasi ya Franka za Cameroon 20,000,000 (Sh 79 milioni) kiasi ambacho wachezaji wa Cameroon wameona ni kidogo na wanashinikiza kulipwa kiasi cha Franka 40,000,000 (Sh 158 milioni).
 
Pamoja na sababu hiyo madai ya bonasi, wachezaji hao wa Cameroon waliandika waraka wa sababu 11 ambazo ziliwasukuma kufanya mgomo huo zikiainisha matatizo yaliyo nyuma ya pazia yanayoligubika soka la Cameroon.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…