Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mara yangu ya kwanza kukutana naye ilikuwa nyumbani kwake jijini Paris, Ufaransa. Alikimbilia kuishi huko baada ya kupigwa pute na kupokonywa urais na Ali Soilih Agosti 3, 1975. Abdalla alipinduliwa na askari wa kukodiwa waliokuwa wakiongozwa na Mfaransa Bob Denard.

Askari haohao wa Bob Denard ndio waliomrejesha Abdallah madarakani Mei 13, 1978, na ndio hatimaye waliomuua.
 
Aliyenipeleka kwa Abdallah alikuwa Amin Ali Moumin al Ahmed, aliyekuwa mwanafunzi wa mahusiano ya kimataifa na ambaye baadaye alikuwa balozi wa muda mrefu wa Comoro katika Umoja wa Mataifa. Amin, aliyekulia na kusoma Zanzibar, alikuwa Mzuwani aliyezaliwa kisiwa cha Nzuwani (Anjouan) ambako ndiko alikozaliwa Abdallah.
 
Tulikuwa na mwenzetu wa tatu aliyefuatana nasi kwenda kwa Abdallah. Alikuwa Nasor Malik, mtangazaji wa BBC niliyekwenda naye Paris kuandaa vipindi maalum vya BBC.

Ingawa ilikuwa ndio mara yetu ya kwanza kukutana, Abdallah akizungumza kana kwamba tukijuana kwa muda mrefu. Dhihaka zake zilivifanya vinywa vyetu vitanuke kwa vicheko.
 
Pamoja na mizaha Abdallah alikuwa na mazito pia ya kuhadithia. Kwanza alitupa siri kwamba katika muda wa miezi sita atarudi Comoro. Hakutuambia atarudi vipi na kusema kweli mimi nilimsikiliza bila ya kumuamini.

Lakini kurudi alirudi, na alirudi mapema zaidi ya alivyotuahidi. Alirudi baada ya miezi mine na si sita. Na siku aliyorudi alinambia kwa simu kwamba anarudi lakini aliniomba niibanie siri hiyo mpaka atapowasili salama Moroni. Sikumvunja.
 
Alinikumbusha yaliyowahi kuwafika Wasudan wawili waliokuwa wanarudi Sudan kutoka London baada ya Rais Ja‘ffer Nimeiry kupinduliwa na Wakomunisti Julai 19, 1971. Mmojawao Luteni-Kanali Babakr al Nur Osman alikuwa ndiye aongoze serikali ya kimapinduzi. Wa pili alikuwa Meja Farouk Hamadallah aliyekuwa awe mjumbe wa Baraza la Mapinduzi, ambalo ndilo lililokuwa litawale.
 
Wote wawili walikuwa London wakitibiwa Nimeiry alipopinduliwa kwa muda mfupi. Kosa walilolifanya walipokuwa wanarudi Khartoum ni kutangaza kwenye mkutano na waandishi wa habari London kwamba wanarudi Khartoum kwa ndege ya shirika la ndege la Uingereza la BOAC.

Libya ilipozipata habari hizo iliilazimisha ndege ya BOAC ilipokuwa juu ya anga ya Libya itue Benghazi. Hamadallah na Osman walikamatwa na baadaye wakasafirishwa kupelekwa Khartoum ambako Nimeiry akiwa amerejea madarakani aliwaua.
 
Abdallah hakutaka yaliyowafika kina Hamadallah yamfike yeye ndipo aliponiomba nisiitangaze safari yake ya kurudi Moroni.

Jambo jengine alilotuambia na lililokuwa likimkera bila ya kiasi ni kuhusu mipango ya hasimu wake Rais Ali Soilih kuifanya Comoro ijiunge na Tanzania. “Hata jina tayari wanalo. Wanataka kuiita nchi hiyo mpya Tanzacomo,” alisema Abdallah.
 
Back
Top Bottom