Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Haftar anaishtumu serikali ya Tripoli kuwa imejaa magaidi na amekuwa akidai kwamba lengo lake ni kuwapiga vita magaidi wote wenye kufuata mielekeo mikali ya Kiislamu kama vile wafuasi wa Dola ya Kiislamu (Islamic State) au Al Qaβ€˜eda. Amekuwa akishtumu kwamba wote wenye kuingiza dini katika siasa ni magaidi wakiwa pamoja n ahata wafuasi wa vuguvugu la Udugu wa Kiislamu (Jami’yat al Ikhwan al Muslimin).
 
The banker ndo imeisha au?
 
Huwa anasahau au labda anajisahaulisha kwamba wengi wenye kumuunga yeye mkono ni watu wenye kufuata misimamo ya Kisalafi ya vuguvugu la Madkhali, lenye kuingiza dini katika siasa. Vuguvugu hilo linajikita juu ya maandishi ya mwanachuoni wa Kisalafi Rabee al Madkhali wa huko Saudi Arabia.

Kwa sasa Haftar anaungwa mkono na Saudi Arabia, Misri, Muungano wa Falma za Kiarabu (UAE), Urussi, Ufaransa na hivi karibuni Rais Donald Trump wa Marekani amejitokeza hadharani kumuunga mkono.
 
Trump ameubadili msimamo wa awali wa Marekani tangu ianze duru hii ya pili ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe huko Libya. Hapo mwanzo sera rasmi ya Marekani ilikuwa kuwa na hadhari na Haftar.

Februari 7 mwaka huu, kamanda mkuu wa majeshi ya Marekani katika Afrika (AFRICOM), Jenerali Thomas Waldhauser, aliishambulia Urussi kwa kujiingiza katika mzozo wa Libya upande wa Haftar. Kuna ushahidi kwamba Urussi na Ufaransa zimekuwa zikimpelekea Haftar wanajeshi wa kukodi na washauri wa kijeshi huko Benghazi. Imekuwa pia ikimsaidia kwa kumpelekea vifaru ya kijeshi, mizinga, ndege za droni na marisawa.
 
Kuna ushahidi kwamba mshauri mmoja mkuu wa Rais Vladimir Putin wa Urussi, Yevgeny Prigozhin, anayejulikana kwa lakabu ya β€œmpishi wa Putin” amekuwa akihusika katika kadhia ya kumsaidia Haftar. Kuna kampuni moja ya Kirussi inayosemekana kumsaidia Haftar kwa kumtengenezea sarafu ili kuisaidia kifedha sehemu ya Libya Mashariki.
 
Urussi, Ufaransa na Marekani ni wazi kuwa zinayarandia mafuta ya Libya. Visima kadhaa vya mafuta mashariki na kusini mwa nchi vimo mikononi mwa wanajeshi wa Haftar.

Kwa upande wao, Saudi Arabia, UAE na Misri hazitaki pawepo serikali ya kidemokrasia ya mwelekeo kama wa Udugu wa Kiislamu nchini Libya. Zinahisi kuwa serikali aina hiyo itawapa funzo baya wananchi wao.

Haftar anataka madaraka tu ya kuwa kiongozi mbabe wa nchi yake. Nafikiri huo uchu wake wa madaraka ndio utaomuangamiza.

hii makala imeandikwa mwezi April 2019
 
Supastaa wa Manchester United, Paul Pogba kwa sasa anauzwa Pauni 150 milioni kwa mujibu wa klabu yake huko Old Trafford, lakini Transfermarkt inatoa orodha yake ya wanasoka wenye thamani kubwa Ligi Kuu England na bei zao halisi wanazopaswa kuuzwa kama kuna timu inahitaji kuwasajili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…