I have learned that people will treat you as you accept to be treated. So if it's not respect don't accept it. If it's not the truth don't accept it, set your standards and don't compromise.
Hata hivyo, hata bei zao pia zimechangamka. Ukitaka mchezaji kutoka Ligi Kuu England basi inakupaswa kuwa vizuri mfukoni. Unaambiwa hivi, kwenye ligi hiyo kuna wachezaji hao ukitaka kuwanunua, basi ni lazima ujihakikishe pesa unayo.
Supastaa wa Manchester United, Paul Pogba kwa sasa anauzwa Pauni 150 milioni kwa mujibu wa klabu yake huko Old Trafford, lakini Transfermarkt inatoa orodha yake ya wanasoka wenye thamani kubwa Ligi Kuu England na bei zao halisi wanazopaswa kuuzwa kama kuna timu inahitaji kuwasajili.
Leroy Sane ameshindwa kupenya kwenye kikosi cha Manchester City na kuwa panga pangua kwenye chama la Pep Guardiola kwa msimu uliomalizika, lakini mara chache alizopata nafasi aliendelea kuonyesha ubora wake ndani ya uwanja.
Jambo hilo limemfanya staa huyo kuwa miongoni mwa wanasoka wenye thamani kubwa huko England, ambapo saini yake inadaiwa kuuzwa Pauni 90 milioni huku Bayern Munich ikiteseka kumpata.
Kiungo wa Tottenham Hotspur, Christian Eriksen amekuwa kwenye klabu hiyo kwa miaka kadhaa sasa na hakika amekuwa mmoja kati ya wachezaji muhimu katika kikosi hicho.
Kutokana na Spurs kumaliza msimu mwingine bila ya kubeba chochote, huku staa huyo mkataba wake ukielekea mwishoni bila ya shaka, Eriksen atafikiria kuondoka kwenye timu hiyo na bei yake ni Pauni 90 milioni.
Thamani ya Kante imekuwa ikipanda kila msimu kutokana na huduma yake bora kabisa ndani ya uwanja na ndio maana kwa sasa bei yake huko sokoni inasema ni Pauni 90 milioni, licha ya kwamba ukienda kutaka huduma yake, lazima Chelsea itahitaji bei kubwa zaidi ili kuzizuia timu zinazotaka kumsajili, zisimbebe.
Paul Pogba alitua Manchester United kwa dili la jumla la zaidi ya Pauni 100 milioni mwaka 2016, wakati ilipomnasa kutoka Juventus.
Kwa muda wake aliokuwa kwenye kikosi cha Man United, huduma ya staa huyo imedaiwa kwamba imeshuka kwa kiasi kikubwa na kumfanya sasa thamani yake kuwa Pauni 90 milioni kwa mujibu wa Transfermarkt.
Bernardo Silva amekuwa na msimu bora kabisa kwenye kikosi cha Manchester City, akiisaidia timu hiyo kubeba mataji yote ya ndani huko England, iliponyakua Ligi Kuu England, Kombe la FA na Kombe la Ligi.
Kiungo huyo huyo ameunda kikosi cha msimu kwenye Ligi Kuu England na alikwenda kutamba pia kwenye Uefa Nations League akiwa na kikosi cha Ureno. Soko linasema bei halisi ya kiungo huyo ukimtaka, basi lipa Pauni 90 milioni.
Sadio Mane alikuwa mmoja kati ya wachezaaji watatu walioshinda Kiatu cha Dhahabu kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita sambamba na Mohamed Salah na Pierre-Emerick Aubameyang.
Mane alisajili dili jipya la kubaki Liverpool kwa muda mrefu hivi karibuni ili kuzipiga marufuku timu zinazomtaka.