Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kama kweli unajali sana afya ya moyo wako, basi pendelea kula korosho za kila aina. Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa kwenye jarida la masuala ya virutubisho nchini Uingereza (British Journal of Nutrition), umeonesha kuwa watu waliopendelea kula korosho na bidhaa zake, kama butter, idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa moyo vilipungua kati ya asilimia 11 na 19.
 
Utafiti huo umeenda mbali zaidi na kubainisha kuwa watu wanaotumia korosho angalau mara nne kwa wiki, walionesha kuondokewa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo (coronary disease) kwa asilimia 37! Na iwapo mtu atakula sana korosho, hatari ya kupatwa na magonjwa huendelea kupungua zaidi.
 
MADINI YA COPPER, UIMARISHAJI MIFUPA, NISHATI
Licha ya kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, korosho pia ni chanzo kizuri cha madini aina ya copper ambayo ni muhimu sana katika mwili wa binadamu. Halikadhalika, korosho ina madini yanayoimarisha mifupa na kinga ya mwili.
 
KOROSHO NA UZITO
Kuna imani potofu kuwa kwa kuwa korosho ina mafuta, ukipenda kuzila basi mlaji huenda akanenepa. Imani hiyo si ya kweli kwani utafiti unaonesha kuwa watu wanaopenda kula korosho, angalau mara mbili kwa wiki, hakuna uwezekano wa kuongezeka uzito na badala yake wanaweza kupungua.
 
Korosho zina faida nyingi kwa afya…ni vizuri kuzijumuisha katika milo kwa sababu baadhi ya manufaa yake ni pamoja na kuwaondolea walaji uwezekano wa kupata maradhi mbalimbali yatokanayo na upungufu wa madini mwilini,” alisema Dk. Abdallah Mwindah wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakati akizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki.
 
Maelezo hayo ya Dk. Mwindah yanalingana kwa kiasi kikubwa na ripoti za majarida mbalimbali ya tafiti za afya, zinazosisitiza kuwa korosho ni chakula muhimu mwilini na pia chenye uwezo mkubwa wa kumkinga mlaji dhidi ya magonjwa kama ya kansa, moyo, uzito mkubwa, mmeng’enyo wa chakula, maradhi yanayohusiana na matatizo ya kupumua na pia kuifanya ngozi ya mlaji wa chakula hicho kwa usahihi kuwa nyororo pasi na mawaa.
 
Faida hizo za korosho, kwa mujibu wa Dk. Mwindah, hupatikana kwa wingi kutokana na kuwa kwake na viinilishe vya madini na vitamini mbalimbali, baadhi vikiwa ni protini, nyuzinyuzi (fibre), vitamini, madini na kemikali za kuondoa vijisumu vyenye kusababisha maradhi ya moyo na maradhi ya damu.
 
UFAFANUZI FAIDA ZA KOROSHO
Akifafanua zaidi jana kuhusiana na faida za korosho, Dk. Mwindah alisema kuwa, tafiti mbalimbali zinabainisha kuwa ulaji wa korosho husaidia utengenezaji wa mbegu za kiume kutokana na kuwa na madini ya zinki.
 
Zinasaidia kuboresha mbegu za kiume na mtu anapokula, humsaidia kuimarisha utimamu wa mwili, mishipa ya fahamu na pia kufanya misuli kufanya kazi yake vizuri kwa kusafirisha damu ipasavyo,” alisema.
 
Aliongeza kuwa, kama mwili utakuwa unafanya kazi vizuri, ni wazi kuwa mhusika atakuwa katika nafasi nzuri ya kushiriki tendo la ndoa kwa sababu pia korosho pia huwa na protini na kuongeza nguvu mwilini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…