Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

*Bodi ya Mikopo*
Nimepita Bodi ya Mikopo leo 20 June kuangalia utekelezaji wao wa kuongeza riba ya 6% kwa deni lililobaki.

1.Ni kweli wanaongeza deni kwa 6% kila mwaka.
2. Deni unaloona kwenye salary slip yako ni Dogo kuliko la kwenye hesabu mpya walizonazo.
3. Hiyo 6% inagawanywa kwa siku 365 na hivyo inaongezwa kila siku.

Mfano unatakiwa kuongezewa 120,000 kwa mwaka, basi ni sawa na elf 10 kila mwezi na ni sawa na sh 333 kila siku ambayo mkopo haujalipwa.
(Hii ina maana balance yako leo sio sawa na kesho)

*Bitter Truth;*
1. Baada ya kukopa, bodi hukata 1% ya mkopo kama processing fee.

2.Baada ya kumaliza chuo, Bodi huongeza riba ya kawaida kwenye mkopo wako.(Kama benki zinavyofanya)

3. Baada ya kukaa mwaka mmoja huongeza riba nyingine inaitwa *penalty*
(Hii ni kwa kuwa umekaa sana na hela yao)
*NB* Ukijumlisha 1-3 hapo juu utapata 55-60 ya deni litakaloongezeka.( _Tuendelee_)

4. Makato yatakuwa 15% ya Mshahara wako kila mwezi.

5. Lakini pamoja na kukukata *processing fees*, *Value Retention fee*, *Penalty* bado wataongeza 6% ya kiasi kilichobaki cha deni lako kwa mwezi husika.

6. Watakata 15% hata kama umevuka ⅓ ya salio la take home.

7. Nakadiria kuwa ukimaliza kulipa, utakuwa umelipa 130%-200% kulingana na ukubwa wa deni lako vs mshahara wako. Hii ni riba ya zaidi ya 100%.

*MyTake*
Bora kukopa Benki ya Biashara, ukasomee,kuliko benki hii[emoji56]
(Yenye Processing, Retention, Penalty, 6% ya ambacho kilishapigwa penalty)

*Mwisho*
Vyama vyetu vya Trade Union n.k kama vile CWT,TUCTA,TRAW n.k vingehangaika usiku na mchana(by book, by hook and by crook) kuhakikisha sheria hii kandamizi na onevu inarekebishwa.

Sio sawa kuongeza 6% kwa deni ambalo umeshaliwekea riba ya kucheleweshwa.

C&P from somewhere!!
 
The company provided a list of criteria that would inform this decision, including "Whether preserving a Tweet will allow others to hold the government official, candidate for public office, or appointee accountable for their statements."
 
"When a Tweet has this notice placed on it, it will feature less prominently on Twitter," the company said, adding that such tweets will not appear in Twitter's algorithmically generated "Top Tweets," its live event pages, and some other features.
 
Sis, unadaiwa na hiyo bodi katili?

Nimesumbuana nao hao kwa muda mrefu na sitaki hata kuwasikia. Walitaka kunibambikiza deni ambalo mwajiri wangu alishalipa na cheti wakampa. Hawafai aisee....
 
Sis, unadaiwa na hiyo bodi katili?

Nimesumbuana nao hao kwa muda mrefu na sitaki hata kuwasikia. Walitaka kunibambikiza deni ambalo mwajiri wangu alishalipa na cheti wakampa. Hawafai aisee....
Wanakera wanatoaga ile barua kuwa umemaliza deni mara ghafla unastuka wameleta deni lingine hii nimeiona kwa watu wengi. Wananidai na nimeapa sitajisalimisha. Mwaka jana nilitaka nilipe kiroho safi nikawapa taarifa zangu hawajaleta makato. Sasa nimeapa sitajisalimisha tena nimeona wanavyotesa watu [emoji16][emoji16].
 
That's my sis [emoji123][emoji123][emoji123][emoji109][emoji109][emoji109]

Mimi walitaka kukikana cheti cha kumaliza deni kuwa eti sio chao nimegushi. Uzuri huwa natunza kumbukumbu vizuri sana na nilikuwa na kila kitu. Mwisho wa siku wakasema yaishe na wakanipa cheti upya. Ila sitashangaa deni lao likiibuka upya...

Wafanyakazi wa bodi ile ni sawa tu na wa TRA au BOT kwa jinsi wanavyotanua. Pesa nje nje...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…