Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baada ya kinywaji hicho kuwalewesha walifikishwa mbele ya Gavana wa Misri ili wapewe adhabu kwa kulewa. Ingawa mwanzoni alisita, lakini alitekeleza adhabu [hadd] kwa kuwachapa bakora na kuwanyoa nywele zao hadharani. Lakini aliitekeleza adhabu hiyo hiyo kwa mmoja wa vijana hao kwa faragha akiwa ndani ya nyumba yake.

Alifanya hivyo kwa sababu kijana huyo alikuwa mtoto wa Seyyidna Omar, ambaye ndiye aliyekuwa Khalifa wa Dola ya Kiislamu wakati huo na ambaye ndiye aliyemteua Amr kuwa Gavana wa Misri.

Alipopata habari hiyo, Seyyidna Omar alimpelekea Amr barua kali ya kumuonya kwa kufanya upendeleo huo na akamtanabahisha kwamba yeye Omar kama kiongozi hampendelei yeyote katika kutimiza wajibu wake.
 
Kisa chengine chenye mafunzo makubwa ni pale mtoto wa Gavana huyo alipompiga kijana mmoja wa Kimisri lakini Amr hakuchukuwa hatua yoyote dhidi ya mtoto wake. Seyyidna Omar alimuita yeye na mtoto wake na baada ya kumkanya akamtaka afanye suluhu na aliyefanyiwa kitendo hicho. Mbali ya hayo, alimwambia maneno ambayo huwa yananukuliwa sana na wapenda uadilifu. Alimwambia: “Hivi wewe ni nani wa kuwafanya watumwa watu waliozaliwa na mama zao wakiwa huru!?”
 
Inawezekana Masauni hafahamu kwa sababu hakuwepo, kwamba masheikh hao hawajawahi kuhusishwa wala kutuhumiwa kisheria kwa makosa aliyoyataja ya kumwagiwa watu tindikali wala kuuawa kwa Padri. Majalada ya kesi hizo yapo na angeweza kujiridhisha. Ni vyema kumtanabahisha kwamba kumsingizia mtu iwe moja kwa moja au vyenginevyo kwa madhumuni tu ya kuonyesha kwamba ni mbaya ni kiwango cha juu cha kukosa uadilifu ambao Masauni anapenda kujinasibisha nao.
 
Hivi Masauni hafahamu kwamba masheikh hao kukaa ndani kwa miaka sita sasa ni adhabu ya kudhiisha na kudhalilisha? Masheikh hao ni watu wenye familia, wenye ndugu, wenye watoto, wenye wanafunzi, wafuasi, majirani na wahisani. Wapo ambao ndoa zao na familia zimeparaganyika kwa sababu tu ya wenyewe kuwa mahabusu. Wapo ambao familia zao zinaishi kwa dhiki kubwa kwa sababu ya wao kutokuwepo. Wapo ambao wazee wao wanaumwa kwa sababu ya fikra juu ya watoto wao.
 
Hakuna asiyejuwa, hata wale wanaojitowa fahamu, kwamba masheikh hao wapo ndani ikiwa sehemu ya uwekezaji unaofanywa kuwanyamazisha wote wanaodai haki zao kama wananchi wa Zanzibar ndani ya Muungano. Na wanafanya hivyo kwa njia ya amani, kwa njia zinazokubaliwa kisheria, njia ya kusema na kutoa mawazo yao. Uwekezaji huo umeanza siku nyingi na bado unaendelea. Hilo ndio kosa walilolifanya na kukamatwa chambilecho Wazungu “red-handed”.
 
Lakini naomba nimtanabahishe Masauni maneno ya mwanasiasa mahiri wa Uingereza Bwana William Pitt [Earl of Catham] aliyoyasema katika Bunge la Uingereza tarehe 14 Januari 1766 wakati akiwatetea na kuwaunga mkono Wamarekani kwa kudai haki zao kutoka kwa Waingereza:

“Gentlemen have been charged with giving birth to sedition in America. They have spoken their sentiments with freedom against the unhappy act, and that freedom has become their crime. Sorry I am to hear the liberty of speech in this House imputed as a crime…I rejoice that America has resisted.”
 
Nadhani Bwana William Pitt anastahiki kujinasibisha na uadilifu kwa kuisema Serikali yake ndani ya Bunge akiwatetea wale ambao wanaoshtakiwa kwa makosa ya uchochezi kwa kudai haki zao huku akionesha wazi kuwa anawaunga mkono katika harakati zao.
 
Aidha, ni vyema Masauni akakumbuka kwamba historia ya dunia imethibitisha kuwa huwezi kutumia nguvu na vitisho kunyamazisha watu wanaodai haki zao. Wenye busara kama vile mbunge mwengine maarufu wa Uingereza, Bwana Edmund Burke, naye katika hotuba yake katika Bunge la Uingereza aliyoitoa Machi 1775 aliitanabahisha Serikali yake kwamba matumizi ya nguvu hayajawahi kusaidia katika kunyamazisha harakati za binadamu kudai haki yake. Yeye alisema: “The use of force is but temporary, it may subdue for a moment, but it does not remove the necessity of subduing again; and a nation is not governed which is to be perpetually conquered.”
 
Inasikitisha sana kwamba katika karne hii ya maendeleo makubwa sana ya binaadamu, katika taifa letu bado wapo viongozi wanaotumia rasilimali na nguvu nyingi kushughulikia mambo ambayo hayaongezi tija wala sifa yoyote kwa taifa. Kama angekuwa na dhamira ya dhati ,Masauni angeisaidia sana Serikali kupata ukweli na ufumbuzi wa suala la masheikh wale wanaoteseka kwa sababu tu ya hakuna aliyepo tayari kuwa mkweli. Watu wote niliowataja na wengine ambao sikuwataja wanaolijuwa suala la masheikh kwa undani wapo na ni wazima wa afya. Mimi naamini kwamba wanaweza kusaidia sana kuueleza ukweli. Baadhi yao wamestaafu na hiyo inawapa fursa ya kuwa wawazi zaidi.
 
Kamara Kusupa na mtambo wa kasumba juu ya Z’bar
Nimesoma katika Gazeti la An-nuur la tarehe 11- 17 Novemba, 2016, makala ya Mwinjilisti Kamara Kusupa isemayo “Kabla ya kudai ‘Fungu Baraka’, ulizeni nani aliitoa Zanzibar UN?” Makala hiyo imeshereheshwa na maneno “tusisahau kila zama na kitabu chake”. Mwandishi wa makala hiyo ameeleza wazi kuwa nia yake ni kujibu makala niliyoandika kuhusu umiliki wa Zanzibar wa kisiwa cha Latham (Fungu Mbaraka) na kusambazwa katika mitandao ya kijamii na magazeti mbali mbali.
 
Katika Makala yake Mwinjilisti Kusupa ameeleza mengi na kutuhumu mengi ambayo yanaonesha kwamba yeye ameichukulia Makala yangu kuwa ya kisiasa, ya kiuchochezi na kwamba ni ishara ya kupinga Muungano. Fikra zake hizi potofu ndio zilizonifanya niweke kumbukumbu sawa.

Aidha, fikra zake hizo potofu zina kila dalili kwamba Mwinjilisti Kusupa ni miongoni mwa mafundi waliobebea wa Mtambo wa Kasumba kuhusu Zanzibar. Unachojua Mtambo huo ni kupotosha kila kitu kuhusu Zanzibar kwa kutumia wino wa usultani na uarabu na kalamu ya Muungano.
 
Jambo la kwanza, Mwinjilisti Kasupa anakiri kuwa haelewi madhumuni ya makala yangu, lakini badala ya kuuliza kama walivyofanya waungwana wengine walionipigia simu kutoka Kigoma, Simiyu, Iringa, Shinyanga, Arusha na Dar yeye ameamua kuchukua wino wake wa usultani na kalamu ya Muungano kuchakata Kasumba.
 
Napenda kumfahamisha kwa ufupi historia na madhumuni ya Makala hiyo. Mwishoni mwa mwaka 2011, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar ilitoa leseni ya uvuvi kwa Kampuni ya Open Water Adventures LTD kwa ajili ya uvuvi wa “sports fishing” katika maeneo ya Zanzibar isipokuwa katika maeneo ya hifadhi ya bahari. Miongoni mwa maeneo ambayo Kampuni hiyo ilikusudia kuvua ni eneo la kisiwa cha Latham (Fungu Mbaraka).

Kampuni hiyo waliomba kuthibitishiwa na Idara ya Uvuvi Zanzibar kuwa eneo la Latham sio sehemu ya hifadhi ya bahari. Idara ya Uvuvi iliwajibu kwa barua yao DFD/2124/II/Vol I ya tarehe 22 Sptemba, 2011 kwamba eneo la kisiwa cha Latham sio eneo la hifadhi ya bahari.
 
Kampuni hiyo ilipeleka wateja wake ambao ni raia wa nchi mbali mbali ikiwemo Marekani na Afrika Kusini kuvua katika kisiwa cha Latham tarehe 16 Novemba, 2011. Wakiwa katika kazi hiyo walikamatwa na watu ambao baadaye walikuja kufahamika kuwa ni maofisa wa Uvuvi wa Tanzania Bara na wakapelekwa Dar es salaam na kuwekwa ndani. Kampuni hiyo pamoja na kutaka ufafanuzi wa uhalali wa kitendo hicho kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ya Tanzania Bara lakini walijibiwa kuwa Wizara hiyo ndiyo yenye mamlaka ya kutoa leseni za uvuvi na kwamba kisiwa cha Latham pia kimo katika mamlaka yao.
 
Baada ya tukio hilo ndipo hatua za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwasiliana na Serikali ya Muungano juu ya kadhia hiyo zilipochukuliwa. Ni kwa kupitia kadhia hiyo ndipo Serikali ya Muungano ilipoamsha rasmi mzozo wa umiliki wa kisiwa cha Latham kwani Waziri Mkuu Mizengo Pinda alieleza wazi kwamba kisiwa hicho kwa mujibu wa kumbukumbu za SMT ni cha Tanzania Bara.
 
Mzozo mwengine wa wazi baina ya pande mbili za Muungano kuhusiana na kisiwa hicho kisiwa ni katika suala la utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia. Ni wazi kwamba suala hili hasa ndio lilopelekea madai ya ajabu ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusiana na kisiwa cha Latham.

Kwa mujibu wa kifungu cha 2 cha Sheria ya Petroli iliyotungwa na Bunge ya mwaka 2015, mafuta na gesi asilia yatasimamiwa na vyombo vya SMT kwa upande wa Tanzania Bara na vyombo na taasisi za SMZ kwa upande wa Zanzibar. Na kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria hiyo mafuta na gesi vitachimbwa katika maeneo ya kijiografia ya Zanzibar na Tanzania Bara. Hata hivyo, si sheria hiyo wala nyengine yoyote iliyofafanua maeneo ya kijiografia ya pande mbili za Muungano.
 
Kisiwa cha Latham mbali ya kuwa kituo kilichotumika kupima eneo la ukanda huru wa kiuchumi wa bahari kuu (baseline point,) lakini kwa ugawaji wa sasa wa vitalu kinaviweka vitalu namba 7, 8 na kitalu cha Latham Kimbiji katika utatanishi mkubwa wa umiliki kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria ya Petroli. Hivyo kupatiwa ufumbuzi wa kitaalamu suala la umiliki wa kisiwa cha Latham sio suala la kasumba ya Kusupa, kwamba ni siasa, bali ni lazima kwa mujibu wa matakwa ya sheria zetu.
 
Jambo la pili muhimu naomba kumrejesha Mwinjilisti Kusupa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Tokea katika Mkataba wa Muungano, suala la kuwepo pande mbili za Muungano na kuwepo Serikali mbili na kuwepo mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano ndio umekuwa mhimili wa Muungano. Ibara ya 4 ya Katiba ya sasa ya Muungano imeliweka jambo hilo bayana sana.
 
Kama unatambua kuwepo mamlaka ya Zanzibar inayoongozwa na Serikali yenye mihimili yote mitatu ya dola, itawezekanaje usibainishe mipaka ya kijiografia ya eneo hilo la kiutawala. Ni kwa mantiki hiyo, ndiyo maana hata Jimbo la uchaguzi, Kata, Shehia, Wilaya na Mkoa yote inayo mipaka ya kijiografia (territorial or geographical boundaries).

Nashindwa kupima nadharia za Mwinjilisti Kusupa anapoona ni dhambi kueleza mipaka ya Zanzibar na anaposema kwamba kusema kwamba kisiwa cha Latham ni cha Zanzibar ni dalili ya kutaka kukitoa kisiwa hicho mikononi mwa Tanzania ili wapewe wageni wafanye wanavyopenda na kuidhuru Tanzania.
 
Jambo la tatu la kumtanabahisha Mwinjilisti Kusupa ni kuwa kwa mujibu wa Sheria za sehemu zote mbili za Muungano, mtu aliyefanya kosa Zanzibar iwe la jinai au madai hawezi kushtakiwa Tanzania Bara na kinyume chake. Hivyo, kwa mfano mtu akitenda kosa la jinai katika kisiwa cha Latham hoja ya mwanzo ni kuwa ashtakiwe katika Mahkama za upande upi na mamlaka ipi ina uwezo wa kumshtaki, DPP wa Zanzibar au wa Tanzania Bara. Hoja hii ipo pia kwa mamlaka za Mahkama na za kiserikali kwa mambo ambayo si ya Muungano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…