Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ni vyema akina Kusupa wakaelewa kwamba hoja ya umiliki sio hoja ya kisiasa wala ya kizayuni, bali ya kikatiba kwa mujibu wa Katiba zetu za Tanzania na ya kisheria kwa mujibu wa sheria zetu za Tanzania. Aidha, hoja ya umiliki wa Latham si ya akina Othman bali ni ya Jahmhuri ya Muungano wa Tanzania.

Serikali ya Zanzibar mara kadhaa imetoa tamko la wazi na bayana ndani ya Baraza la Wawakilishi ambalo limekuwa likidai ufafanuzi wa umiliki wa kisiwa hicho. Katika maelezo yake, Serikali imekuwa siku zote ikiwatoa hofu Wazanzibari kuwa kisiwa hicho ni cha Zanzibar na hakuna anayeweza kukidai. Matamko ya karibuni yametolewa na waliopo sasa madarakani kupitia Bwana Mohamed Aboud na Bwana Issa Haji Ussi Gavu wote wametoa kauli hizo katika Baraza la Wawakilishi. Wote hao wawili ni mawaziri katika utawala uliopo Zanzibar na ambao naamini akina Kusupa hawana mashaka nao juu ya utii wao kwa TANZANIA.
 
Mbali ya matamko hayo ndani ya Baraza la Wawakilishi, hivi karibuni, ndani ya Bunge la Muungano Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Januari Makamba alijibu suali kuhusu kisiwa cha Latham. Kituko alichofanya ni kuwa alisema kuwa kisiwa hicho ni cha Muungano wakati aliulizwa kuwa jee kisiwa hicho kipo upande gani wa Muungano. Naamini kama angeulizwa kuhusu kisiwa cha Mafia asingesema kuwa kisiwa hicho ni cha Muungano. Waswahili wanasema “mwenye macho haambiwi tazama”. Kwa wenye macho wanaona bila kuambiwa kuwa kuna mgogoro baina ya pande mbili za Muungano.
 
Lakini kama kawaida Tanzania ya zama za kitabu cha akina Kusupa kila kitu kinafichwa, kinapotoshwa na kupambwa kwa siasa za dahri na zama. Ni baada ya majibu hayo, ndipo nilipoamua kuwaeleza ukweli Watanzania juu ya suala hilo. Hivyo, ni dhahiri mtambo wa kasumba wa akina Kusupa haufurahii na ukweli huo na wanatafuta kila njia kuzalisha kasumba za kupotosha ukweli.
 
HOJA YA MIKATABA YA ZAMANI NA MIPAKA YA WAKOLONI

Mwinjilisti Kusupa amepotosha kiasi cha kupotosha au niseme amejipotosha mno kuhusu suala la mikataba ya kikoloni na mipaka ya leo ya nchi za Afrika. Kwa fikra zake kwamba mikataba ya kikoloni iliyoigawa Afrika haina nafasi sasa hivi. Na haifai kutumika kujenga hoja. Ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa akina Othman hawana tofauti na wenye chachu ya kizayuni wanaotumia maandiko ya kale kuhalalisha anayofanya sasa hivi. Nasema amejipotosha kwa vile katika makala hiyo anakubaliana na Tamko la OAU la 1963 kuhalalisha mipaka ya kikoloni.
 
Suala ni kuwa jee Mwinjilisti Kusupa anajua kuwa mipaka ya kikoloni ilitumia maandiko ya kale zaidi kuliko 1898 wakati Zanzibar ilipotangaza rasmi kuwa Latham ni ya kwake? Aidha, Kusupa anajenga dhana kwamba ni mipaka ya Zanzibar tu ndiyo iliyoundwa na Sultani lakini ile ya Tanganyika ni ya kizalendo na imeakisi matakwa ya Watanganyika wenyewe.
 
Labda nimtanabahishe Mwinjilisti Kasupa tu kwamba, kwanza, mipaka ya eneo la Afrika Mashariki ambalo baadaye lilikuja kuwa Tanganyika kama nchi moja, ilianza hasa na utashi wa mtu mmoja, Carl Peters, kinyume hata na matakwa ya viongozi wa nchi yake ya Ujerumani. Wanahistoria wanaelewa vizuri kwamba Kansela wa Ujerumani wa wakati huo, Bwana Otto von Bismark, ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa kwa mfalme wao William II, hakuwa na hamu na sera ya makoloni Afrika
 
Ni baada ya ushawishi wa Carl Peters na wenzake na kuonesha kwa vitendo kuwa tayari wanazo sehemu wanazoweza kuzifanya makoloni Afrika, ndipo ramani ya iliyokuja kuwa Tanganyika ilipoanza kuchorwa kuanzia tarehe 3 Machi 1885 wakati Emperor William wa Ujerumani alipokubali kuyatambua maeneo yaliyopatikana kwa mikataba ya ghilba ya Carl Peters na machifu wenyeji. Maeneo yaliyotambuliwa yalikuwa manne tu; nayo ni Usagara, Naguru, Useghu na Ukami [inawezekana maeneo hayo sasa yamebadili majina].
 
Kutambuliwa huko kulipata nguvu baada ya Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza, Bwana Glanville, alipomueleza Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Count Herbert von Bismarck, kwamba Uingereza inatambua maeneo hayo ya Ujerumani katika bara ya Afrika Mashariki. Wakati Tanganyika inaanza kuchorwa na Wajerumani, Zanzibar tayari ilikuwa na mikataba ya kibalozi na Marekani, Uingereza, Italia, Ufaransa na Ubelgiji. Takriban nchi zote hizo zilikuwa na balozi zao Zanzibar. Marekani, kwa mfano, chini ya Balozi wao ambaye alikuwa pia alikuwa mfanyabiashara, Bwana Richard Waters, ilikuwa ikifanya biashara kubwa na Zanzibar wakati huo.
 
Ni baada ya hatua hiyo ya Mfalme William na hatua ya Uingereza kutambua mbegu iliyozaa Tanganyika, ndipo Balozi wa Ujerumani aliyekuwepo Zanzibar, Dk. Gerhard Rohlfs, alipomtaka Sultani naye atambue rasmi maeneo ya Ujerumani ya Bara. Sultani alipokataa ndipo mwezi wa Agosti 1885 kikosi cha Wanamaji cha Ujerumani kilipopelekwa Zanzibar kumtishia Sultani kuitambua mipaka ya Ujerumani huko Bara au wangelitumia nguvu. Hatua hii iliifanya Uingereza iingilie kati na kumshawishi Sultani akubali mipaka hiyo [ingawa kumbukumbu zinaonesha Ujerumani na Uingereza shauri lao lilikua moja].
 
Tarehe 14 Agost 1885, Sultani alikubali mipaka hiyo na Tume ya kuainisha mipaka ikaundwa na kuanza kazi Oktoba mwaka huo wa 1885. Hatimaye, baada ya Tume ya Mipaka kumaliza kazi, ilipelekea Mkataba wa 1886 baina ya Uingereza na Ujerumani kuhusiana na kuainisha mipaka ya Ujerumani Bara na Mipaka ya Zanzibar. Ujerumani ilichukua takriban eneo lote ambalo leo ndio Tanganyika na Zanzibar ikabakishwa na ukanda wa pwani wa Bara wa maili 10 tokea Mto Ruvuma hadi Mto Tana.
 
Sina hakika kama Mwinjilisti Kusupa itapotokea mzozo wa eneo la Tanganyika, ataukubali mkataba huo wa 1886 au kwake utakuwa ni uzayuni kutumia maandiko ya kale kuhalalisha haki yako ya sasa.

Baada ya mkataba huo wa 1886, Tanganyika ilikuja kuwekwa bayana zaidi na mkataba wa Heligoland- Zanzibar wa Julai 1890. Mkataba huu pia ndio uliweka bayana zaidi mipaka ya Kenya na Uganda za leo.

Ukifatilia harakati na matokeo yaliyopelekea mkataba wa Heligoland, ni wazi kuwa ulizingatia zaidi maslahi ya Wajerumani na Waingereza na sio ya makabila kadhaa ambayo kwa wakati huo yalikuwa bado hayajawa nchi moja.
 
Ni baada ya kuondoka Kansela Otto von Bismark madarakani Machi 1890, ndipo Waingereza walipoingia hofu kuwa Mfalme William angelifuata ushawishi wa wafanyabiashara na wanasiasa wanaopenda Ujerumani iwe na sehemu kubwa ya makoloni Afrika. Ushahidi wa hofu hii ya wazi ya Waingereza ilioneshwa na jarida la TIMES la tarehe 20 Machi 1890, ambapo lilieleza kuwa Waingereza wengi wanapenda iwepo suluhu ya mipaka ya makoloni Afrika baina ya Uingereza na Ujerumani ili kuepusha ugomvi baina ya Uingereza na Ujerumani utaotokana na uchu wa makoloni wa Ujerumani baada ya Bismark kuondoka.
 
Ni kutokana na hilo ndipo Sir Percy Anderson wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza alipotakiwa aende Berlin, Ujerumani, kuanzisha mazungumzo na Serikali ya Kansela Leo von Caprivi aliyeshika madaraka baada ya Bismark. Kabla ya kwenda Berlin, Anderson alionana na Balozi wa Ujerumani nchini Uingereza, Count Hatzfeldt, na hatimaye akaenda Ujerumani tarehe 3 Mei 1890 na kuanza mazungumzo tarehe 5 Mei 1890 na Dk. Krauel wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani.
 
Mazungumzo hayo yalizaa majadiliano ya miezi 2 ambapo kila upande ukieleza kile inachotaka. Ujerumani ikikubali kuitoa sehemu ya Ziwa Nyanza upande wa kaskazini lakini ikishikilia nayo kuachiwa Ukanda wa Pwani uliopo chini ya Zanzibar na kisiwa cha Heligoland. Mjadala mkali katika Bunge la Uingereza wa 22 Mei 1890 unatoa ufafanuzi wa kutosha juu ya maslahi ya wakoloni kwa mipaka waliyochora.
 
Hatimaye mkataba wa Heligoland- Zanzibar ulitiwa saini tarehe 1 Julai 1890, lakini ulihitaji kuidhinishwa na Mabunge ya Uingereza na Ujerumani. Mkataba huo ndio uliokuja kuiondoa Ruvuma, Mtwara, Lindi, Mafia, Dar es Salaam na Tanga na sehemu ya mwambao wa pwani wa Tanganyika kutoka mikononi mwa Zanzibar. Mjadala mkali katika Bunge la Uingereza wakati wa kujadili Mswada wa Sheria ya Kuiondoa Heligoland Uingereza (Heligoland Cessation Bill) uliofanyika tarehe 3 Julai 1890 na hotuba ya Kansela Leo von Caprivi katika Bunge la Ujerumani la Reichstag tarehe 28 Julai 1890 ni ushahidi wa kutosha kwamba Afrika Mashariki iligaiwa kwa kuzingatia maslahi ya kiuchumi na kimkakati ya wakoloni.
 
Aidha, ni ushahidi kuwa mipaka ya Tanganyika na Zanzibar haikuwekwa na Sultani bali na Waingereza na Wajerumani. Ni ushahidi pia kwamba mipaka ya leo ni ajali ya kihistoria ambayo tumekuja kuikubali kama ilivyo na kuilinda kwa Katiba, Sheria na nguvu zetu za kijeshi kama tulivyofanya kule Kagera.

Ni vyema pia akina Kusupa wasome kwa makini kitabu cha Map of Africa by Treaty kilichoandikwa na Sir Edward Hertslet ambacho ndicho kinachotumiwa kama rejea ya kuthibitisha mipaka ya Afrika katika Mahkama za kimataifa na Mabaraza ya Usuluhishi ya mipaka. Sina hakika kama Kusupa atawaita wanaotumia kitabu hicho ni Wazayuni kama anavyowaita akina Othman.
 
Jambo la mwisho kuhusu mikataba ya zamani na mipaka ya Afrika na dunia napenda kumtanabahisha Kusupa kuwa hata sheria za kimataifa zimetambua Treaty Law kama msingi mkuu wa kuamua mipaka baina ya nchi mbalimbali duniani. Na katika mikataba inayotambulika na sheria za kimataifa ile mikataba ya zamani inapewa uzito wa aina ya pekee. Aidha, sheria za kimataifa zinatambua mipaka iliyowekwa wakati wa ukoloni kuwa ni msingi mkubwa wa uhalali wa mipaka ya sasa. Chini ya Kanuni ya Uti Possidetis, hata Mahkama ya Kimataifa ya ICJ mara kadhaa imeipa uhalali mipaka ya kikoloni katika kuamua migogoro ya mipaka Afrika, Amerika ya Kusini na Asia.
 
Kwa hili la Latham lipo jambo la ziada la kuzingatia. Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1963 ilieleza wazi kwamba mipaka ya Dola ya Zanzibar ni visiwa vya Unguja, Pemba na Latham. Katiba hiyo ndiyo iliyotumika na Zanzibar kuomba na kukubaliwa uanachama wa Umoja wa Mataifa. Aidha, wakati huo Tanganyika ilishatangulia kupata uhuru kwa angalau miaka miwili. Haikutokea hata siku moja, Tanganyika kulalamika rasmi au kwa njia isiyo rasmi kwamba mipaka hiyo ya Zanzibar inaingilia Tanganyika.
 
Akina Kasupa wanapojaribu kutuuzia kasumba kwamba mipaka hiyo ni ya Sultani kwa vile tu inahusu Zanzibar kama kwamba ile ya Tanganyika na nchi nyengine za Afrika ni mipaka ya kizalendo, ni kudhihirisha kwamba wanadhani Watanzania na hasa Wazanzibari hawawezi kupambanua ajali hiyo ya historia ambayo tumeihalalisha na madam tumeikubali na kuihalalisha ni lazima tuilinde kama tulivyoilinda Kagera bila kujali udugu wa Waganda na Watanzania wa Kagera. Aidha, ajali hiyo ya kihistoria kama tulivyobainisha imetambuliwa na sheria na Mahkama za Kimataifa na pia Umoja wa Nchi Huru za Afrika na Tanzania ndio iliyokuwa kinara wa azimio hilo la OAU la kutambua mipaka ya kikoloni.
 
HOJA YA SULTANI NA UMILIKI WA ZANZIBAR

Kusupa anajaribu kutuuzia kasumba nyengine ya ovyo zaidi anaposema kwamba Latham ni ya Sultani sio ya Wazanzibari na hivyo hawawezi kuidai. Nasema hii ni kasumba ya ovyo kwa vile kwa ushahidi nilioeleza hapo juu, sio tu kuwa Tanganyika ni ya Wajerumani lakini kwa ajali hiyo hiyo ya historia ilikuwa ya Zanzibar na ikachukuliwa kwa hila na nguvu na Wajerumani. Hivi kuna mtu yeyote wa Tanganyika au Mtanzania wa leo aliyehusika kuweka mipaka ya Tanganyika? Kama ni hivyo, msingi gani uliotumiwa na Tanzania kupigania Kagera?
 
Back
Top Bottom