Ripoti zinadai kwamba kipa huyo mkongwe yupo kwenye hatua za mwisho kabisa za kurejea kwenye klabu yake hiyo ya zamani ya Juventus baada ya kumalizana na Paris Saint-Germain.
Paolo Maldini ndiye anayeshikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi kwenye Serie A baada ya kuitumikia AC Milan mara 647, mechi saba nyuma ya Buffon alizocheza kwenye ligi hiyo.
Kipa huyo sasa, Buffon anataka Juventus wamchezesha walau kwenye mechi nane msimu ujao ili ang'atuke kwenye soka akiwa amecheza mechi 648 kwenye Serie A na kuweka rekodi.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 41 alikuwa akihusishwa na mpango wa kujiunga na Barcelona kabla ya wababe hao wa Nou Camp kumsajili Neto kutoka Valencia. Baadaye ikaibuka taarifa kwamba anasakwa na Leeds United inayocheza kwenye Championship.
Kilichopo kwa sasa ni juu ya Juventus kukubali au kukataa matakwa hayo ya Buffon hasa ukizingatia kwamba kwa sasa wamekuwa na imani kubwa sana na kipa wao Wojciech Szczesny.
Lakini, taarifa mpya zinadai kwamba kocha mpya wa wababe hao wa Turin, Maurizio Sarri anapiga hesabu za kumsajili Pepe Reina, aliyewahi kuwa naye Napoli.
Maajabu ya Mwenyezi Mungu ndani ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, mito miwili inapokutana na kuwa mto mmoja bila maji yake kuchanganyikana. Mto KASAI na mto MAYINDOMBE.
Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, ameiomba klabu yake ya Crystal Palace imruhusu ahamie Arsenal. Palace inamthaminisha streka huyo streka huyo kuwa na thamani ya pauni milioni 80. (Mirror)