Jonathan Benteke
Mdogo wa staa wa kimataifa wa Ubelgiji, Christian Benteke. Baada ya Benteke mkubwa kununuliwa kwa dau la pauni 32 milioni na Crystal Palace, ambalo lilikuwa dau la rekodi, Palace waliamua kumchukua na mdogo wake Jonathan ambaye ndiye kwanza mkataba wake ulikuwa umechanwa na klabu ya S.V. Zulte Waregem ya Ubelgiji.