Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1562255224997.jpeg
 
Mtu aliyekuwa akihusika na usajili kwenye kikosi hicho cha The Gunners, Dick Law, alifunga na kusema winga hiyo pamoja na kipa Thibaut Courtois miongoni mwa orodha ya wachezaji wa viwango vya dunia ambao Arsenal ilishindwa kuwasajili kwa sababu tofauti tofauti, lakini kubwa ubahili.
 
Kuhusu Ronaldo alikwenda hadi kufanya mazoezi kwenye timu hiyo wakati huo akiwa na umri wa miaka 18. Kwa mujibu wa Law, shida kubwa kwenye klabu hiyo ilikuwa ukosefu wa pesa, hivyo walijikuta wakizidiwa na wapinzani kwenye dili za kuwanasa wachezaji hao.
Mtu huyo alikuwa akisimamia usajili kuanzia mwaka 2005 hadi 2018 alisema: “Ilikuwa ngumu sana.
 
Law alisema waling'ata meno kwa Thibaut Courtois na kufahamu kwamba ni kipa mzuri, lakini shida ilikuwa kwenye mkwanja.
Mkuu wa maskauti Steve Rowley na mkurugenzi mtendaji mkuu Ivan Gazidis ndio waliokuwa watoa uamuzi wakubwa sambamba na Wenger kwenye suala la usajili wa mchezaji. Na hapo Law alisema mapendekezo yake ya kusajiliwa wakali hao yalikosa nguvu kama mabosi hao watatu watakuwa wameweka 'no'.
 
Pesa si kwamba haikuwapo, shida tulikuwa tunaogopa kujaribu. Kutumia pesa nyingi kwa mchezaji mmoja kisha asicheze vizuri, tuliogopa hiyo hasana. Tulikosa vipaji vingi sana. Nakumbuka tulivyokaa na Steve, Ivan na Arsene kumjadili Thibaut Courtois. Hata Eden Hazard pia, lakini hatukuwasajili.”
 
Nyota wengine ni Kylian Mbappe, Paul Pogba, N'Golo Kante na Raphael Verane, ambao wanatengeneza kikosi hicho matata kabisa, kingekuwa kinabeba mataji kila msimu, hata Ligi ya Mabingwa Ulaya, taji ambalo Arsenal inalisikia tu kwa wenzao.
 
Back
Top Bottom